Mwanaharakati Mzalendo

STARS YAPOTEZA MCHEZO WAKE WA KWANZA UGENINI KIMAGUMASHI

 

MWAMUZI wa kati ya timu ya taifa ya Tanzania iliyokuwa inamenyana na Libya nchini Tunsia leo amebeba furaha ya mashabiki kwa kufanya maamuzi yasiyo ya kungwana mbele ya Stars nchini Tunisia.

Mchezo wa leo umekamilika kwa Stars kupoteza kwa kufungwa mabao 2-1 licha ya kuanza kufunga bao la kwanza dakika ya 18 kwa mkwaju wa penalti kupitia Mbwana Samata baada ya Msuva kuchezewa rafu.

Dakika ya 68 mwamuzi alitoa penalti ya kungaunga kwa Libya jambo lililowavunja moyo wapambanaji wa Stars kwenye mchezo wa kuwania tiketi ya Afcn nchini Tunisia na bao likapachikwa na Sand Masoud dakika ya 68 ambaye alipiga penalti.

Dakika ya 81 zikiwa zimebaki dakika 9 mpira kukamilika Anias Saltou aliandika bao la pili akiwa ndani ya 18 kutokana na safu ya ulinzi kufanya makosa ya wazi.

Mchezaji wao tegemeo kwa Libya, Hamdou Mohamed alionyeshwa kadi nyekundu dakika ya 87.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *