Mwanaharakati Mzalendo

UONGOZI SIMBA WATOA TAMKO JUU YA KIBARUA CHA PATRICK AUSSEMS


Ofisa Mtendaji wa klabu ya Simba, Senzo Mazingisa, amesema Kocha Mbelgiji, Patrick Aussems alimtumia ujumbe ukimwarifu kuwa amepatwa na dharura.

Taarifa imesema kuwa Aussems alimtumia Mazingisa ujumbe huo lakini hakuanisha kuwa ameelekea wapi japo inalezwa alisafiri kuelekea kwao Ubelgiji.

Mazingisa amesema Aussems hakumwambia kuwa anaelekea wapi na ameahidi kulitolea ufafanuzi zaidi pale atakaporejea nchini.

“Aussems bado ni mwajiriwa katika klabu ya Simba.

“Alinitumia ujumbe Jumatatu kuwa ana dharura lakini hakueleza kuwa anaelekea wapi, akisharejea nitakuwa na ya kueleza,” amesema Mazingisa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *