Mwanaharakati Mzalendo

Upande Wa Utetezi Kesi Ya Kutekwa Kwa ‘Mo’: “Upelelezi Unachelewa”

Upande wa utetezi katika kesi ya tuhuma za kutekwa kwa Mfanyabiashara Mo Dewji umeulalamikia upande wa mashtaka kwa kuchelewesha upelelezi wa kesi hiyo inayomkabili dereva wa taxi Mousa Twaleb na wenzake wanne ambao bado hawajakamatwa.
Malalamiko hayo yametolewa na wakili wa utetezi Maufudhu Mbagwa katika Mahakama ya Kisutu mbele ya Hakimu Mkazi Huruma Shaidi wakati kesi hiyo ilipokuja kwa ajili ya kutajwa.
Wakili huyo amedai hadi sasa mwaka mmoja umepita tangu mteja wake awekwe mahabusu na hajaambiwa hatua ya upelelezi wa kesi hiyo ulipofikia.
Kesi imeahirishwa hadi November 24 mwaka huu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *