Mwanaharakati Mzalendo

Waliompiga Risasi RPC Mwanza Wahukumiwa Kunyongwa Hadi Kufa

Mahakama Kuu kanda ya Mwanza imewahukumu kunyongwa hadi kufa, washtakiwa wanne baada ya kupatikana na hatia ya mauaji ya aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza Liberatus Barlow October, 2012.
Hukumu hiyo imetolewa Mwanza na Jaji Sirialus Matupa baada ya Mahakama kuridhika kuwa Watuhumiwa hao wanne kati ya saba walitenda kosa hilo.
Waliohukumiwa kunyongwa hadi kufa ni Muganyizi Michael, Magige Mwita, Abdallah Petro na Abdulrhaman Ismail.
Kamanda Barlow aliuawa kwa kupigwa risasi eneo la Kitangiri Wilayani Ilemela Mwanza, saa 8 usiku wa kuamkia October 13,2012.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *