Mwanaharakati Mzalendo

WAZEE YANGA WATAKA CHEO CHA NUGAZ KIFUTWEKufutia kuibuka kwa sintofahamu baina ya Antonio Nugaz na Hassan Bumbuli juu ya nyadhiza zao, imeelezwa wazee na baadhi ya wadau wa Yanga wametaka cheo cha Ofisa Uhamasishaji kifutwe.

Taarifa zinaeleza kuwa wazee na wadau hao wameona hakuna haja ya kuwepo kwa cheo hicho kutokana na kutokuwepo kwenye katiba ya klabu hiyo.

Mapendekezo haya yankuja kufutia wawili hao, Nugaz na Bumbuli kila mmoja kujiita ni Ofisa Habari wa klabu nafasi ambayo amepewa Bumbuli.

Ikumbukwe Nugaz hivi karibuni alipewa cheo cha Uofisa Uhamasishaji ndani ya Yaga ambayo wazee hao wameona haina haja ya kuwepo na hii ni baada ya kutofautiana kwa kauli baina yao wawili.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *