Mwanaharakati Mzalendo

HII NDIYO HATUA YA MCHAKATO WA MABADILIKO ILIPOFIKIA YANGAMwenyekiti Mkuu wa klabu ya Yanga, Dr. Mshindo Msolla, amesema kuwa kamati maalum inayohusika na mchakato wa mabadiliko inaendelea vizuri.

Msolla ameeleza kuwa kwa sasa kamati hiyo inaendelea na kazi vema na kufikia mwezi Mei mwakani kila kitu kitakuwa kimekamilika.

Mwenyekiti huyo ambaye bado hajatimiza mwaka tangu achaguliwe ndani ya uongozi huo, ameeleza kwa kuwataka wanayanga wawe na subira hivi sasa kila kitu kitaenda kama kilivyopangwa.

“Mchakato wa mabadiliko unaenda vizuri.

“Kamati ambayo ambayo inahusikana na suala hili imefikia pazuri na inaendelea na kazi.

“Tunawaahidi kufikia mwezi Mei mwakani kila kitu kitakuwa kimeenda sawa.”


CHANZO ; SALEHE JEMBE


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *