Mwanaharakati Mzalendo

MASHABIKI WA SIMBA WAFUNGUKA BAADA YA PATRICK AUSSEMS KUFUTWA KAZI

Baada ya klabu ya Simba SC kupitia Bodi yake kuthibitisha kumfuta kazi kocha Patrick Aussems  baada ya kushindwa kutekeleza majukumu kwa viwango na malengo ambayo walikubaliana naye kwenye mkataba wa ajira.

Mashabiki wa Simba wamefunguka na kusema kuwa Aussems ni kocha bora huku wakishusha lawama kwa viongozi wao kuwauza baadhi ya wachezaji na kusajili wachezaji ambao awana viwango.

“Kwangu mimi Patrick
Aussems atabakia kuwa kocha bora kabisa kuwahi kutokea kwenye klabu yetu ya Simba na ligi nzima ya Tanzania. Huu ujinga viongozi mmemuangushia jumba bovu kocha utamuuzaje okwi unamsajili Kanda? Utamuuzaje Kotei ukamsajili Fraga?” Jay C Yrn.

“Sikufurahishwa hata kidogo na maamuzi haya,  Hao hao waliotoa maamuzi ndio hao hao walionunua wachezaji wa kibrazil bila kumshirikisha kocha ambao kwa sasa ni mzigo na hawana kiwango chochote, Tunachokitafuta, tutakipata tusipojipanga vizuri” Albert Machua.

“Patrick Aussems ni kocha bora sana kwangu ila mpira wa nchi yetu unazengwe sana, japo klabu ya Simba inajitaidi kuendesha kisasa ila kuna mambo bado kidogo, nenda salama Aussems ndio maisha ya makocha ndio changamoto zao nje ya uwanja” Salum Manyamba.

“Si tunataka ushindi tu hatakama kutakua hakuna kocha. Mimi kama shabiki nahitaji ushindi mengine watajua wenyewe” Mfaume Abdallah Msoma.

Kupitia kwenye ukurasa wa mtandao wa Twitter kocha Patrick Aussems amethibitisha kuwa amepokea barua ya kufutwa kazi ya kuifundisha klabu ya Simba SC kwa kuandika ujumbe uliosomeka “Bodi ya Wakurugezi kupitia kwa Mtendaji Mkuu (CEO) imenitaarifu kuwa mimi siyo kocha Mkuu wa Simba”.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *