Mwanaharakati Mzalendo

QUEEN DARLEEN AOLEWA KIMYA KIMYA MWENYEWE AFUNGUKA.

Mwanamuzuki,  Darleen ambaye yupo chini ya WCB, amefunga ndoa kimya kimya na mfanyabiashara wa magari jijini Dar es Salaam alifahamika kwa jina moja la Isihaka, ndoa hiyo iliyofungwa siku ya Jumapili na kuhudhuliwa na ndugu jamaa na marafiki.

Akizungumza kupitia kipindi cha Block89, kinachorushwa na kituo cha radio Wasafi FM, Queen Darleen amesema ni kweli ameolewa, na anamshukuru Mungu.

“Ni kweli nimeolewa Namshukuru Mwenyezi Mungu amenijalia, ndoa sio lazima uposti mitandao kuwa umeolewa”.

” Ndoa zimeanza kabla ya mitandao. Swala hili la ndoa nimelifanya mimi na mume wangu na familia yangu, kikubwa swala limeenda salama” alisema Queen Darleen.

Baadh ya watu mbalimbali wakiwepo wasanii wenzake kutoka WCB wamempongeza na kumtakia kila la kheri katika maisha yake ya ndoa na mume wake huku wakimtaka kuwa uvumilivu na mwenye upendo.

“Mwenyezi Mungu akusimamie kwenye maisha yako mapya ya ndoa dada Dareen…..mdogo wako nimefurahi sana kushuhudia hili….Nakuombea Amani, Upendo na Utulivu vitawale na uviipembe kipaumbele, Ndoa yako Mwenza wako…. Amiin Rabbillalaamin”  Mbosso.

“Sijui nilie jana (Jumapili) nimekosea ila tunairudia hongera sana ndugu yangu dadaangu, Mungu akubariki katika ndoa yako akuepushie  na husda za walimwengu yani daaah Mungu ni mwema shemu langu nakupenda sina cha kusema wallah Queen Darleen jisebedue wakuone ridhiki mafungu saba” Esma Platnumz.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *