Mwanaharakati Mzalendo

SAMATTA NDANI YA KAMPUNI MPYA YA UWAKALA

Mbwana Samatta hatimae ameondoka katika kampuni ya uwakala ( First For Players) aliyojiunga mwaka 2018 na kujiunga na Spocs Consultant inayomsimamia Mohamed Salah mchezaji wa timu ya Liverpool inayoshiriki ligi kuu England.

Hatua hiyo inamfanya Samatta kuwa mchezaji wa pili mwenye thamani ya juu kwa wanaosimamiwa na kampuni hiyo baada ya Mohamed Salah.

Samatta anashika nafasi ya pili katika list ya wachezaji zaidi ya 100 wenye  thamani kubwa wanaosimamiwa na kampuni hiyo ya Spocs Consultant.

Samatta anashika nafasi hiyo ya pili kwa kuwa na thamani ya pound milioni 12 kwa mujibu wa mtandao wa transfer Market, anaamini kufanya huko na uzoefu wa kampuni hiyo mpya kunaweza kusaidia ndoto yake ya kucheza EPL.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *