Chombo cha anga ya juu cha China kinachoitwa Chang’e kimeanza tena kazi yake ya uchunguzi kwa siku ya 15 ya mwandamo baada ya kulala wakati wa usiku wa baridi kali.
Sehemu ya kutua ya chombo hicho iliamka saa 12:57 asubuhi Jumanne, na sehemu ya kuzunguka iliamka saa 11:55 jioni Jumatatu.
Habari zilizotolewa na Kituo cha uchunguzi wa mwezini na angani cha taifa la China, sehemu hizo zote mbili ziko katika hali nzuri ya utendaji kazi.
Sehemu ya kuzunguka iitwayo Yutu-2 imesafiri mita 367.25 upande wa mbali wa mwezi, ikiwa na mpango wa kwenda kaskazini magharibi kisha kusini magharibi kuendelea na uchunguzi wa kisayansi.