Dodoma itakuwa na umeme mwingi kupita mikoa yote nchini – Waziri Kalemani – Mwanaharakati Mzalendo
ADVERTISEMENT
  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact
Mwanaharakati Mzalendo
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv
No Result
View All Result
Mwanaharakati Mzalendo
No Result
View All Result
Home HABARI

Dodoma itakuwa na umeme mwingi kupita mikoa yote nchini – Waziri Kalemani

Mhariri by Mhariri
Feb 20, 2020
in HABARI
0 0
0
Dodoma itakuwa na umeme mwingi kupita mikoa yote nchini – Waziri Kalemani
0
SHARES
76
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Serikali kupitia Wizara ya Nishati, inakamilisha mradi mkubwa wa upanuzi wa kituo cha kupoza umeme kilichopo Zuzu Dodoma, ambacho baada ya kukamilika kitakuwa na uwezo wa megawati zaidi ya 600, hivyo kuongoza Tanzania nzima kwa wingi wa umeme.

Hayo yamebainishwa na Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani, jana Februari 19, 2020 alipofanya ziara katika kituo hicho kujionea maendeleo ya utekelezaji wa mradi husika.

Akizungumza na waandishi wa habari, Waziri amebainisha kuwa, kwa kiasi hicho cha umeme (megawati 640), Dodoma italipita hata jiji la Dar es Salaam ambalo linaongoza kwa sasa kwa kuwa na megawati takribani 587. “Napenda niishukuru sana Serikali kupitia kwa Mheshimiwa Rais kwa kutupatia Dola za Marekani milioni 52 kwa ajili ya kutekeleza mradi huu,” amesema.

Akifafanua zaidi kuhusu manufaa ya mradi huo, Dkt Kalemani amesema mbali na kutosheleza mahitaji ya kawaida ya wananchi, kiasi hicho cha umeme pia kitawezesha uwekezaji wa viwanda vya aina mbalimbali hivyo kukuza uchumi.

Ameeleza zaidi kuwa, dhamira ya serikali kutekeleza mradi huo ni kutokana na ongezeko la mahitaji ya umeme mkoani humu ambayo yamepanda kutoka wastani wa megawati 15 hadi kufikia megawati 40 kwa siku.

Amesema, ongezeko hilo la mahitaji linaweza kusababisha uhaba wa nishati ya umeme Dodoma endapo hazitachukuliwa hatua za makusudi na haraka katika kulitafutia ufumbuzi na kuongeza kuwa, ndiyo maana serikali imeagiza mradi huo ukamilike na kukabidhiwa ifikapo mwishoni mwa mwezi huu wa Februari, 2020.

“Kasi ya kuongezeka kwa shughuli za kiuchumi Dodoma ni kubwa. Tukizembea, hali inaweza kuwa mbaya, jambo ambalo serikali haiwezi kuruhusu litokee.

Kufuatia umuhimu wa kukamilika kwa mradi huo mapema, Waziri amemtaka mkandarasi anayetekeleza mradi huo, kampuni ya KCE kutoka India, kufanya kazi usiku na mchana ili akamilishe kazi kwa wakati huku akisisitiza kuwa kamwe hataongezewa muda.

ADVERTISEMENT

Katika hatua nyingine, Waziri ameuagiza uongozi wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), kupitia kwa Msimamizi wa Mradi husika, Mhandisi Peter Kigadye, kushughulikia malalamiko ya wananchi wanaoishi jirani na kituo hicho.

 

ADVERTISEMENT
Mhariri

Mhariri

Related Posts

Wakusanya ushuru wa huduma wapigwa msasa
HABARI

Wakusanya ushuru wa huduma wapigwa msasa

by Mhariri
Jan 21, 2021
0

Nteghenjwa Hosseah,Singida Mkurugenzi Msaidizi wa Fedha Idara...

Read more
Viongozi wanne kizimbani kuuza aridhi kinyume na sheria

Viongozi wanne kizimbani kuuza aridhi kinyume na sheria

Jan 21, 2021
Waziri Mkuu aagiza na tozo za Mkonge zifanyiwe mapito

Waziri Mkuu aagiza na tozo za Mkonge zifanyiwe mapito

Jan 21, 2021
Zaidi ya Bilioni 800 kutumika ujenzi wa miundombinu ya maji nchini.

Zaidi ya Bilioni 800 kutumika ujenzi wa miundombinu ya maji nchini.

Jan 20, 2021
Bweni lililochomwa moto 2018 laungua tena,kura zapigwa kubaini mhusika

Bweni lililochomwa moto 2018 laungua tena,kura zapigwa kubaini mhusika

Jan 20, 2021
Waziri Jafo aagiza shule ya Msingi Nkuhungu kufanyiwa ukarabati haraka

Waziri Jafo aagiza shule ya Msingi Nkuhungu kufanyiwa ukarabati haraka

Jan 20, 2021
Next Post
Watu 20 wafariki India kwa ajali ya Basi kugongana na Lori

Watu 20 wafariki India kwa ajali ya Basi kugongana na Lori

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

I agree to the Terms & Conditions and Privacy Policy.

Currently Playing

KRANTZ MWANTEPELE (FOUNDER & CEO)

ADVERTISEMENT

KONCEPT TV

https://www.youtube.com/watch?v=0HP0mB_rtIU&t=7s
ADVERTISEMENT
Mwanaharakati Mzalendo

Mwanaharakati Mzalendo ni mtandao namba moja kwa habari makini kutoka pande zote za dunia kuhusiana na Michezo, Siasa, Afya, Elimu, Mahusiano, Vituko, n.k

Wasiliana nasi kwa Email;krantzcharles@gmail.com
SIMU; 0658123310

Follow Us

February 2020
M T W T F S S
« Jan   Mar »
 12
3456789
10111213141516
17181920212223
242526272829  
Currently Playing
  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

All rights reserved © 2020 Mwanaharakati Mzalendo - Powered by Koncept.

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv

All rights reserved © 2020 Mwanaharakati Mzalendo - Powered by Koncept.

Login to your account below

Forgotten Password?

Fill the forms bellow to register

*By registering into our website, you agree to the Terms & Conditions and Privacy Policy.
All fields are required. Log In

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In