Kikosi cha mabingwa wa Tanzania timu ya Simba kimewasili salama jijini Mwanza asubuhi hii tayari kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wa kombe la Azam Sports Federation Cup dhidi ya Stand United utakaopigwa Jumanne katika uwanja wa Kambarage mkoani Shinyanga.
Simba imeondoka alfajiri hapa jijini Dar es Salaam kwa usafiri wa ndege ikiwa na kikosi chake kizima ambapo kitakuwa Mwanza kwa mazoezi ya siku chache kabla ya kuelekea Shinyanga.
Kwa mujibu wa ukurasa maalum wa Instagram wa mabingwa umethibitisha kikosi hicho kufika salama ikiambatana na picha za wachezaji wakiwasili jijiji Mwanza.
Wekundu hao jana waliibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Biashara United katika mchezo wa ligi kuu uliopigwa uwanja wa Taifa.