[pl_row] [pl_col col=12] [pl_text]
Mwaka huu, Tigo imedhamini tena mbio hizi maarufu za Tigo Kili Half Marathon (Km 21) ikiwa ni mara ya tano mfululizo, ili kutoa fursa kwa watanzania na watu kutoka nchi jirani kushiriki, kubadilishana tamaduni,kuburudika na kufurahi kwa pamoja
. Mbio hizi zitafanyika Tarehe 1, Machi katika Chuo cha Ushirika hapa mjini Moshi.Tigo tunafarijika kuwa washirika wa mbio hizi kubwa na za aina yake ambazo zitawakutanisha wadau mbalimbali wakiwamo Viongozi wa Serikali na taasisi,wanariadha wa ndani na nje ya nchi, pamoja na wananchi kutoka maeneo mbalimbali.
Sote tunatambua umuhimu wa mashindano haya hasa kwa washiriki na Taifa kwa ujumla kuwa mbali na kujenga afya ya mwili, mbio hizi zinasaidia kuchochea shughuli za kiuchumi kupitia biashara, kukuza utalii pamoja na kuhamasisha utunzaji wa mazingira.
Hii ni fursa kwa kila mtanzania kushiriki kwenye mbio hizi kubwa hapa nchini, tunapenda kuwahamasisha watanzania wengi zaidi kujiunga kwani mashindano ya mwaka huu yatakuwa na msisimuko wa aina yake.
Ningependa pia kuchukua fursa hii kuwambia wafanyabiashara wote wakae mkao wa kula,kwani mwaka huu tunatarajia wageni zaidi elf 15,kuwasili hapa Moshi,kwani kuna watakao kimbia,na ambao watakao kuja kuwashangilia wanaokimbia,na pia wale ambao watakuja kikazi kama waandaji wa mbio hizi.
Usajili wa wakimbiaji umeshakamilika(5,500), watu watachukua namba zao za kukimbilia: -Dar/Mlimani City/22/23 Februari 2020 -Arusha/Kibo Palace Hotel/25/26 Februari 2020 -Moshi/Key Hotel(Urdu road)/27/28 Februari 2020 Kusafiri kwa Reli kuelekea Moshi wakitokea Dar es Salaam.
Vile vile vikundi vya jogging club,pamoja na washindi waliojinyakulia nafasi ya kushiriki mbio hizi watasafiri kuja Moshi tarehe 28/kufika 29 asubuhi kwa train. Tutawapokea kwa mbwembwe asubuhi watakapo wasili.
Washindi
Katika mbio hizi, Tigo inatoa zawadi za kifedha zenye thamani ya Shilingi Milioni 11 kwa washindi 10 wa kwanza wa Kili Half Marathon(wanawake na wanaume).Pia,washiriki 5,500 watakaomaliza Km 21 watapewa medali za heshima.Vilevile, tutatoa vyeti kwa washiriki wote wa Kili Half Marathon.
Tungependa kuwaatarifu wateja wetu kwamba wateja wetu wataweza kuwatumia marafiki, ndugu na jamaa, matukio mbali mbali matukio yatakayokuwa yanaendelea siku hio kupitia mtandao wetu ulioboreshwa kupitia mitandao ya kijamii kwa kutuma picha na video kupitia intaneti ya kasi ya 4G+.
KAULI MBIU: UJANJA NI KUFUTA VILIMA
[/pl_text] [/pl_col] [/pl_row]