Watu 20 wakiwemo wanawake watano wamepoteza maisha yao na wengine 28 kujeruhiwa leo Alhamisi nchini India baada ya basi walilokuwa wakisafiria kugongana na lori katika jimbo la Tamil Nadu, kusini mwa nchi hiyo,
Waziri wa usafiri katika jimbo la Kerala A.K. Saseendran amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo.
Kwa mujibu wa Saseendran, gurudumu moja la basi hilo lilipasuka na kusababisha dereva kupoteza udhibiti wa gari kisha likagongana na lori hilo lililokuwa likiendeshwa upande mwingine wa barabara kwa mwendo wa kasi zaidi.
Hivi sasa, wafanyikazi wa shirika la usafiri wa barabarani jimboni Kerala (KSRTC) wamekimbia kwenye eneo hilo kufanya uchunguzi na kuwasilisha ripoti ya ajali hiyo.