Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo amewataka viongozi wa Wilaya ya Karatu kuhakikisha ujenzi wa hospital ya Wilaya ya Karatu kuwa wa Mfano kwa kuwa itakua inatoa huduma kwa wageni wa nje ya Nchi na wenyeji wa Wilaya hiyo.
Waziri Jafo ametoa agizo hilo wakati alipotembea ujenzi wa Hospital hiyo inayoendelea kujengwa katika Kata ya Daa, kijiji cha Changarawe na Tarafa ya Karatu.
Waziri Jafo amesema “nimefurahishwa na maendeleo ya ujenzi wa hospitali hii na katika mwaka huu wa fedha tumetenga shilingi milioni 500 kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa hospitali hii.
“Fedha hizo zikija kwa kuwa mmeshajenga majengo matatu ya awali angalieni majengo mengine ya kipaumbele ndio myajenge kwa fedha hizo mhakikishe hospitali hii inakamilika tena kwa ubora”. alisema.
Waziri Jafo aliongeza kuwa Hospitali hii itakapokamilika nataka tulete vifaa tiba vyote vinavyohitajika ili muweze kutoa huduma bora kwa wananchi lakin hata na wataliii ambao wamekua wakifika hapa Karatu kwa ajili ya kwenda kwenye vivutio vya Utalii.
“Sio mtalii akipata tatizo kidogo tu la Afya ni mpaka apelekwe Arusha Mjini hilo sasa tutalimaliza kwa kuwa na hospitali nzuri na yenye huduma bora ili watalii hao wapatiwe huduma katika Hospital hii ya Karatu’ alisema Jafo.
Naye Mbunge wa Karatu Mhe. William Kambalo amesema ni mategemeo ya wananchi wa Karatu kuona hospital hiyo inakamilika na inatoa huduma inayostahiki kwa afya ya wana karatu wote.
Wakati huo huo Mwenyekiti wa Halmadhauri ya Karatu Mhe. Lazaro Gege ameahidi kuzisimamia fedha zote zitakazoletwa kwa umakini wa hali ya juu ili kufikia lengo la kupata Hospitali ya Mfano ya Wilaya.
Naye Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Waziri Moris amesema wameshapikea shilingi milioni 500 kutoka Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro ambazo zimetumika kujenga majengo matatu ambayo ni Jengo la Wagongwa wa Nje (OPD), Jengo la Utawala pamoja na maabara na kuwa ujenzi wa hospital utaendelea kadiri fedha zinavyoendelea kupatikana.