CORONA VIRUS: DStv yapanua wigo wa habari, elimu na burudani kwa wateja wake – Mwanaharakati Mzalendo
ADVERTISEMENT
  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact
Mwanaharakati Mzalendo
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv
No Result
View All Result
Mwanaharakati Mzalendo
No Result
View All Result
Home BIASHARA

CORONA VIRUS: DStv yapanua wigo wa habari, elimu na burudani kwa wateja wake

Enock Mambya by Enock Mambya
Mar 24, 2020
in BIASHARA, HABARI, HABARI TANZANIA
0 0
0
CORONA VIRUS: DStv yapanua wigo wa habari, elimu na burudani kwa wateja wake
0
SHARES
146
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Ni katika jitihada za kuhakikisha jamii inapata habari za uhakika, elimu ya kutosha na burudani kipindi hikicha mapambano dhidi ya corona

Pamoja na changamoto iliyopo duniani kwa sasa, MultiChoice inawahakikishia wateja wake wa DStv kuwa inayazingatia mahitaji yao has ukizingatia kuwa kwa sasa watu wengi wanalazimika kukaa nyumbani katika jitihada za kuzuia maambukizi ya virusi vya corona.

“Tutaendelea kukupa wigo mpana zaidi wa kupata habari za uhakika kwa kufungua chaneli za habari kwenye vifurushi vyetu. Tunazingatia mawasiliano ya mara kwa mara na mamlaka husika na tutashiriki kikamilifu katika kupambana na kuenea kwa ugonjwa wa Covid-19. Ni muhimu sana sote tuzingatie maelekezo na maagizo yanayotolewa na mamlaka sahihi na wataalamu wetu ili kuhakikisha kuwa tunalinda afya zetu na za wenzetu” amesema Jacqueline Woiso, Mkurugenzi Mtendaji wa MultiChoice Tanzania

Mkurugenzi huyo ametangaza rasmi kwamba kuanzia sasa;

• Fahamu kinachoendelea
Ili kukuwezesha kupata habari na taarifa za uhakika katika kipindi hiki, tunapanua wigo wa habari kwa kufungua chaneli kubwa za habari katika vifurushi vyetu. Kuanzia leo chaneli ya CNN (401) na Euronews (414) zitafunguliwa kwa wateja wa vifurushi vyote kuanzia kile cha chini kabisa cha DStv Bomba. Pia tumefungua chanel maarufu ya habari za Afrika Africanews (chaneli 417) kwenye vifurushi vyetu vyote hadi tarehe 1 Mei ambapo chaneli hii itakuwa inapatikana kuanzia kifurushi cha DStv Family.

• Kwa watoto
Kwa kuzingatia kuwa Watoto wetu wako likizo kipindi hiki, maudhui ya elimu yamezingatiwa ambapo chaneli ya elimu ya Da Vinci (Chaneli 318) na ile ya burudani ya Cartoon Network (channel 310) sasa zimefunguliwa kwa vifurushi vyote kuanzia cha chini kabisa cha DStv Bomba. Hii ni katika jitihada za kuhakikisha watoto wetu wanaendelea kupata elimu na burudani wakati huu wakiwa nyumbani.

ADVERTISEMENT

• Michezo
Kama unavyofahamu, matangazo mubashara ya michezo mbalimbali yameathiriwa sana kwani michezo mingi sasa hivi imesitishwa. Hata hivyo ili kuhakikisha kuwa hutindikiwi na burudani kipindi hiki ambacho unashauriwa kupunguza mizunguko na safari zisizo za lazima, tunakuletea Makala maalum za michezo (sport documentaries) kutoka kila pembe ya dunia pamoja na kuonyesha matukio makubwa ya kimichezo yaliyotokea siku za nyuma. Pia chaneli maarufu ya michezo SuperSport1 (201) sasa imefunguliwa katika kifurushi cha DStv Compact na DStv Compact Plus. Chaneli hii itakuwa na matukio yaliyoweka rekodi katika ulingo wa michezo duniani. Kwa wale wapenzi wa mbio za magari wataburudika na chaneli ya SuperSport7 (207) ambayo imefunguliwa kwa vifurushi vyote.
Huduma kwa wateja:
Tunajali afya za wateja na wafanyakazi wetu, katika kipindi hiki cha tahadhari tumeandaa utaratibu ambapo baadhi ya wafanyakazi watafanya kazi wakiwa nyumbani. Hii ina maana kuwa kunaweza kukawa na kuchelewa kupata huduma. Hata hivyo tuna njia nyingi mbadala za kidijitali – kimtandao ambapo mteja anaweza kupata huduma nyingi kwa urahisi na ufanisi zaidi.

Huduma hizo ni pamoja na ; My DStv App inayopatikana kwenye Google Play na App Store, IVR – huduma ya sauti iliyorekodiwa, Huduma ya WhatsApp kwa namba 0677 666 111 ambapo unaweza kufanya malipo, kubadili kifurushi, kuangalia salio na huduma nyingine muhimu. Pia unaweza kupiga simu Huduma kwa wateja kupitia namba +255 222 199600 na +255 784 104 700, Tovuti : www.dstv.com, USSD: *150*53# pamoja na huduma ya ujumbe mfupi SMS kwenda 15727

Kwa wewe unayetaka kufungiwa huduma ya DStv wakati huu, fahamu kuwa mafundi wetu wote wamechukua tahadhari kubwa kuhakikisha kuwa wanafanya kazi kwa usalama. Mafundi wamepewa mahitaji muhimu na maelekezo rasmi ya kuchukua tahadhari wakati wa kutoa huduma.

Mabadiliko ya ratiba
Kutokana na hali hii ya dharura, michezo mingi imeathirika. Athari hizi pia zimezikumba tasnia nyingine za michezo na burudani kama vile uzalishaji wa filamu. Tutakuwa tukiwajuza wateja wetu kuhusu mabadiliko ya ratiba kadiri yatakavyokuwa yanatokea. Pi unaweza kutembelea www.dstv.com

ADVERTISEMENT
Enock Mambya

Enock Mambya

Journalist | Digital Media Enterpreneur | Subscribe and Follow us

Related Posts

Hotuba ya mwisho ya Trump
HABARI

Hotuba ya mwisho ya Trump

by Ombeni Osward
Jan 20, 2021
0

Rais wa 45 wa Marekani, Bwana  Donald...

Read more
Nyaraka za Serikali kuandikwa kwa Kiswahili

Nyaraka za Serikali kuandikwa kwa Kiswahili

Jan 20, 2021
Rwanda kutoa chanjo ya homa ya Nguruwe ili kuzuia maambukizi

Rwanda kutoa chanjo ya homa ya Nguruwe ili kuzuia maambukizi

Jan 20, 2021
TIGO YAKABIDHI ZAWADI KWA WASHINDI WA WAKALA PUSH PROMOTION KWA MAWAKALA WA MIKOANI

TIGO YAKABIDHI ZAWADI KWA WASHINDI WA WAKALA PUSH PROMOTION KWA MAWAKALA WA MIKOANI

Jan 20, 2021
Wagonjwa wapya wa saratani waongezeka Tanzania

Wagonjwa wapya wa saratani waongezeka Tanzania

Jan 20, 2021
Mfumo wa TEHAMA wa kufuatilia utendaji wa mizani, barabara, viwanja vya ndege, karakana na vivuko

Mfumo wa TEHAMA wa kufuatilia utendaji wa mizani, barabara, viwanja vya ndege, karakana na vivuko

Jan 20, 2021
Next Post
TANZIA: Mwanamuziki Manu Dibango afariki kwa Virusi vya Corona

TANZIA: Mwanamuziki Manu Dibango afariki kwa Virusi vya Corona

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

I agree to the Terms & Conditions and Privacy Policy.

Currently Playing

KRANTZ MWANTEPELE (FOUNDER & CEO)

ADVERTISEMENT

KONCEPT TV

https://www.youtube.com/watch?v=0HP0mB_rtIU&t=7s
ADVERTISEMENT
Mwanaharakati Mzalendo

Mwanaharakati Mzalendo ni mtandao namba moja kwa habari makini kutoka pande zote za dunia kuhusiana na Michezo, Siasa, Afya, Elimu, Mahusiano, Vituko, n.k

Wasiliana nasi kwa Email;krantzcharles@gmail.com
SIMU; 0658123310

Follow Us

March 2020
M T W T F S S
« Feb   Apr »
 1
2345678
9101112131415
16171819202122
23242526272829
3031  
Currently Playing
  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

All rights reserved © 2020 Mwanaharakati Mzalendo - Powered by Koncept.

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv

All rights reserved © 2020 Mwanaharakati Mzalendo - Powered by Koncept.

Login to your account below

Forgotten Password?

Fill the forms bellow to register

*By registering into our website, you agree to the Terms & Conditions and Privacy Policy.
All fields are required. Log In

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In