Huduma ya App ya kutuma video ya China, TikTok jana iliwaalika wajasiriamali kujiunga na shindano la kwanza duniani la kutoa mawazo yao ya biashara.
Meneja operesheni ya maudhui wa TikTok katika timu ya Afrika Boniswa Sidabwa, amesema kwenye taarifa kwamba waanzilishi wote wa makampuni mapya yaliyo katika hatua ya awali wa Afrika na Mashariki ya Kati wanapaswa kuwasilisha mawazo yao ya uvumbuzi kwa video ya dakika moja ambayo itaeleza na kuvutia jopo la majaji duniani kabla ya Septemba 24.
Sidabwa amesema mpango huo wa ufadhili utawapatia wajasiriamali fursa ya kushindania uwekezaji wenye thamani ya dola za Kimarekani 10,000 na kupatiwa ushauri na Mfuko wa Gritti kwa mwaka mmoja.
Zaidi ya hapo washindi watatu wa mwanzo watazawadiwa nafasi ya pekee ya kushiriki mchezo wa kuruka angani sambamba na kumalizia kuwasilisha mawazo yao kwa hatua ya mwisho.