Mkali wa Vitasa tokea Mkoani Morogoro Twaha Kiduku amesema Yupo tayari kuingia Uringoni na Bondia Bingwa Tanzania kwasasa Hassan Mwakinyo ili kudhihirishia Watanzania ni nani Mbabe kati yao .
Akizungumza kupitia Spoti Arena, Wasafi FM Twaha amesema kuwa pambano kati yake na Mwakinyo licha ya kuwa Litakuwa kivutio kwa Watanzania Wengi, Lakini Pia litamuongezea heshima Mwakinyo kama akifanikiwa Kumpiga .
Mpaka sasa Mabondia hao wanashikiria Nambari 2 za Juu katika Ranks za Masumbwi Nchini , Mwakinyo akiwa namba 2 na Twaha Kiduku akishika Namba 2 .
Hivyo ni dhahiri kuwa endapo pambano hilo likitokea, basi litakuwa ni Pambano la Kumtafuta Mfalme wa Msumbwi Tanzania.