Wateja wa Vodacom M-Pesa Kunufaika na Gawio la Bilioni 3.5 za Faida ya M-Pesa – Mwanaharakati Mzalendo
ADVERTISEMENT
  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact
Mwanaharakati Mzalendo
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv
No Result
View All Result
Mwanaharakati Mzalendo
No Result
View All Result
Home BIASHARA

Wateja wa Vodacom M-Pesa Kunufaika na Gawio la Bilioni 3.5 za Faida ya M-Pesa

I am Krantz by I am Krantz
Sep 10, 2020
in BIASHARA
0 0
0
Wateja wa Vodacom M-Pesa Kunufaika na Gawio la Bilioni 3.5 za Faida ya M-Pesa
0
SHARES
73
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter
ADVERTISEMENT

10 Septemba 2020, Dar es Salaam: Wateja wa Vodacom M-Pesa takribani milioni 8, kuanzia leo watapata sehemu ya faida ya shilingi bilioni 3.5 ikiwa ni gawio kutoka kwenye akaunti ya M-Pesa Trust. Kampuni ya Vodacom Tanzania PLC imetangaza kwamba kuanzia leo wateja wake wa M-Pesa watapata sehemu yao ya gawio hilo lililopatikana kama faida ya matumizi ya huduma hiyo.
Akizungumza na waandishi wa habari, Mkurugenzi wa M-Commerce Epimack Mbeteni alisema, “tuna shauku ya kugawana faida hii na wateja wetu kwani wao ndio sababu ya mafanikio ya huduma ya M-Pesa. Huduma ya M-Pesa imechangia maendeleo lukuki ya watanzania na mpango huu umedhamiria kuendelea kuwapa wateja wetu faida zaidi. Wateja wote wa Vodacom ambao wamekuwa wakitumia M-Pesa kuanzia Januari mosi hadi Machi 31 mwaka huu watafaidika na bonus hii ya shilingi bilioni 3.5 ambayo itagawiwa moja kwa moja kupitia M-Pesa”.
Kuanzia sasa wateja wa Vodacom wanaweza kutuma SMS ya neno KIASI kwenda namba 15300 ili kujua kiwango gani cha faida watapokea. Baada ya kupata gawio hili, wateja wa M-Pesa wanaweza kukomboa faida hiyo kwa kuitoa kama fedha taslimu, kununua muda wa maongezi, vifurushi au kulipia bili.
“Kiasi ambacho mtu atapokea kama sehemu ya faida hiyo itategemea na idadi ya miamala aliyokuwa akifanya kwa kipindi nilichotaja hapo juu. Shughuli hizo ni kama miamala ya kuhamisha fedha, malipo ya bili mbalimbali au manunuzi ya muda wa maongezi. Napenda kuwahimiza wateja wetu kutuma SMS ili kujua ni kiasi gani cha gawio hili wanastahili kupokea,” alisisitiza Mbeteni huku akiongeza kwamba mpaka sasa Vodacom Tanzania PLC imeshagawa faida ya jumla ya shilingi bilioni 133 kwa wateja wa M-Pesa.
M-Pesa ina umiliki wa soko wa asilimia 39 na inaongoza kwa kuwa huduma ya fedha za mkononi inayotumiwa na watanzania wengi zaidi ambao wanafanya miamala ya hadi Shilingi bilioni 100 kwa siku. “Tumewekeza vilivyo katika M-Pesa ndani ya miaka kumi na mbili iliyopita na sasa huduma imekuwa na ufumbuzi wa kibunifu unaokidhi mahitaji ya watanzania kupitia bidhaa mbalimbali kama vile M-Koba, M-Pawa, Halal Pesa M-Pesa MasterCard na nyingine nyingi. Tunaendelea kuwa na nia ya kuboresha huduma hii kwa njia ya ubunifu huku tukishirikiana na makampuni pamoja na wavumbuzi mbalimbali ili kuendesha ajenda ya ujumuishwaji wa kifedha nchini,” alimaliza Mbeteni.

ADVERTISEMENT
I am Krantz

I am Krantz

Related Posts

Tigo yazindua huduma ya ‘Lipa Kwa Simu’
BIASHARA

Tigo yazindua huduma ya ‘Lipa Kwa Simu’

by I am Krantz
Jan 19, 2021
0

Huduma hii ya malipo, sasa itafahamika kama...

Read more
PATA PATA NA TIGO YAKABIDHI MILIONI 10 KWA WASHINDI WAWILI

PATA PATA NA TIGO YAKABIDHI MILIONI 10 KWA WASHINDI WAWILI

Jan 12, 2021
Arise B.V (Arise) inamiliki 34.9% ya hisa zilizokuwa za Rabobank katika Benki ya NMB ya Tanzania.

Arise B.V (Arise) inamiliki 34.9% ya hisa zilizokuwa za Rabobank katika Benki ya NMB ya Tanzania.

Jan 8, 2021
Jumla ya Shilingi Milioni 20 Zimeshatolewa katika Promosheni ya kila wiki ya NMB MastaBATA

Jumla ya Shilingi Milioni 20 Zimeshatolewa katika Promosheni ya kila wiki ya NMB MastaBATA

Jan 5, 2021
Vodacom Tanzania PLC yatwaa Tuzo ya kwanza ya uandaaji bora wa taarifa za Fedha kwa mwaka 2019

Vodacom Tanzania PLC yatwaa Tuzo ya kwanza ya uandaaji bora wa taarifa za Fedha kwa mwaka 2019

Jan 5, 2021
Vodacom yatamatisha kampeni ya Shangwe Shangwena kwa kukabidhi gari Dodoma

Vodacom yatamatisha kampeni ya Shangwe Shangwena kwa kukabidhi gari Dodoma

Jan 4, 2021
Next Post
RAS Simiyu ataka majengo ya upasuaji, wodi ya wazazi Hospitali ya wilaya Busega yakamilishwe

RAS Simiyu ataka majengo ya upasuaji, wodi ya wazazi Hospitali ya wilaya Busega yakamilishwe

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

I agree to the Terms & Conditions and Privacy Policy.

Currently Playing

KRANTZ MWANTEPELE (FOUNDER & CEO)

ADVERTISEMENT

KONCEPT TV

https://www.youtube.com/watch?v=0HP0mB_rtIU&t=7s
ADVERTISEMENT
Mwanaharakati Mzalendo

Mwanaharakati Mzalendo ni mtandao namba moja kwa habari makini kutoka pande zote za dunia kuhusiana na Michezo, Siasa, Afya, Elimu, Mahusiano, Vituko, n.k

Wasiliana nasi kwa Email;krantzcharles@gmail.com
SIMU; 0658123310

Follow Us

September 2020
M T W T F S S
« Aug   Oct »
 123456
78910111213
14151617181920
21222324252627
282930  
Currently Playing
  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

All rights reserved © 2020 Mwanaharakati Mzalendo - Powered by Koncept.

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv

All rights reserved © 2020 Mwanaharakati Mzalendo - Powered by Koncept.

Login to your account below

Forgotten Password?

Fill the forms bellow to register

*By registering into our website, you agree to the Terms & Conditions and Privacy Policy.
All fields are required. Log In

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In