Bia ya Serengeti Lager yasaini mkataba wa bilioni 3 kuidhamini Taifa Stars – Mwanaharakati Mzalendo
ADVERTISEMENT
  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact
Mwanaharakati Mzalendo
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv
No Result
View All Result
Mwanaharakati Mzalendo
No Result
View All Result
Home BURUDANI

Bia ya Serengeti Lager yasaini mkataba wa bilioni 3 kuidhamini Taifa Stars

I am Krantz by I am Krantz
Oct 6, 2020
in BURUDANI, MICHEZO
0 0
0
Bia ya Serengeti Lager yasaini mkataba wa bilioni 3 kuidhamini Taifa Stars
0
SHARES
63
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter
ADVERTISEMENT

 

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bia ya Serengeti Mark Ociiti (aliyeshika mfano wa hundi kushoto) akiwa pamoja na Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo (kati kati aliyeshika mfano wa hundi) Dr Hassan Abbas pamoja rais wa TFF Wallace Karia muda mfupi baada ya Bia ya Serengeti Lager kusaini mkataba wa miaka mitatu wenye thamani ya Tshs 3bn/-wa kuidhamini Taifa Stars . Kulia ni wawakilisi kutoka TFF na kushoto ni wafanyakazi wa Serengeti.



Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bia ya Serengeti Mark Ociiti (wa kwanza kulia) akiimsikiliza mkurugenzi wa sheria wa kampuni hiyo Lucia Minde (wa pili kulia) na mwanasheria wa TFF Rahim Shaban (wa tatu kulia) akimwelekea jambo rais wa TFF Wallace Karia huku Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo  Dr Hassan Abbas akishuhudia utiaji saini wa mkataba kati ya TFF na Bia ya Serengeti kuidhamini timu ya Taifa.


Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bia ya Serengeti Mark Ociiti akiongea wakati  Bia ya Serengeti Premium Lager ilipotangaza kuongeza udhamini wake kwa timu ya taifa kwa miaka mingine mitatu jijini Dar es Salaam.



Baadhi ya wachezaji wa Timu ya Taifa, Taifa Stars waliohudhuria hafla ya kutiliana mkataba kati ya TFF na Bia ya Serengeti Premium Lager ambapo bia hiyo ilipotangaza kuongeza udhamini wake kwa timu ya taifa kwa miaka mingine mitatu jijini Dar es Salaam.


Na Mwandishi Wetu 

Bia ya Serengeti Premium Lager (SPL) leo imeingia makubaliano na kusaini mkataba na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kwa ajili ya kuidhamini Timu ya Taifa, Taifa Stars kwa kipindi kingine cha miaka mitatu.

Mkataba huo unaogharibu shilingi bilioni 3 za Kitanzania, umesainiwa baada ya ule wa awali uliosainiwa mwaka 2017, kufikia ukomu kati kati ya mwaka huu huku timu ikijivunia mafanikio mengi katika kipindi cha udhamini.

Akizungumza wakati wa utiaji saini wa mkataba huo mpya uliofanyika jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa SBL Mark Ocitti alisema kuwa, bia ya Serengeti Premium Lager ni mdau mkubwa wa michezo hapa nchini na kuongeza kuwa bia hiyo imekuwa ikijivunia kuwaunganisha Watanzania kupitia michezo.

“Kupitia bia yetu pendwa ya Serengeti Premium Lager, tunayo furaha kubwa kutangaza leo kutangaza udhamini kwa Timu yetu ya Taifa kwa kipindi kingine tena cha miaka mitatu. Tumechukua uamuzi huu kwa kuzingatia na kufahamu umuhimu wa michezo kwenye maendeleo ya kijamii na kiuchumi. Tunaamini kwa kuidhamini Taifa Stars, siyo tu tunachangia katika maendeleo ya michezo bali pia tunachangia kukuza mpira wa miguu ambao watu wengi duniani na Tanzania wanaupenda sana,” alisema Mark 

Mkurugenzi huyo aliongeza, “Tumeamua kusaini tena mkataba huu baada ya kuridhishwa na maendeleo pamoja na mafanikio ya timu kwa miaka mitatu iliyopita lakini pia kutoka na mapenzi makubwa ya Watanzania kwa timu yao ya taifa,”

Taifa Stars imefanikiwa kupata mafanikio makubwa chini ya udhamini uliomalizika wa bia ya Serengeti Premium Lager ikiwa ni pamoja na kuweza kufuzu na kucheza mashindano makubwa barani Afrika ya Mataifa ya Afrika (AFCON)  mwaka jana ikiwa ni baada ya miaka 39 tangu kushiriki mara ya mwisho.

Udhamini huu mkubwa unakuja katika kipindi ambacho biashara nyingi katika ngazi ya kitaifa na kimataifa zinapunguza udhamini kwenye shughuli mbali mbali zikiwamo za kimichezo pamoja na kupuguza gharama za uendeshaji kutokana na janga la Corona ambalo limerudisha nyuma maendeleo ya biashara na mzunguko wa fedha duniani.

Akiishukuru bia ya Serengeti kwa udhamini huo, Rais wa TFF Wallace Karia alisema fedha zilizotolewa kwa ajili ya udhamini huo zitatumika kama ilivyokusudiwa na kuongeza kuwa zitasaidia sana katika kufanikisha uendeshaji ya timu na hivyo kupata matokeo mazuri katika michezo yake.

Kusainiwa kwa mkataba huu leo ni Ushahidi wa wazi kuwa bia ya Serengeti Lager ina imani ya kutosha na uongozi wa TFF na tunaahidi kuwa tutasimama imara kutumia udhamini huu kama mkataba unavyosema kwa manufaa ya timu yetu ya Taifa,” aliongeza Karia

Udhamini huu ni muendelezo wa bia ya Serengeti Premium Lager kuiunga mkono timu ya taifa, baada ya kufanya hivyo katika kipindi cha kati ya mwaka 2010 na 2012 na katika kipindi cha mkataba uliomalizika mwaka huu wa miaka mitatu na ambao ulisainiwa mwaka 2017.

MWISHO……………

Tags: TAIFA STARS
ADVERTISEMENT
I am Krantz

I am Krantz

Related Posts

Lacazette ananisaidia kuongeza ujasiri – Smith Rowe
HABARI

Lacazette ananisaidia kuongeza ujasiri – Smith Rowe

by Ombeni Osward
Jan 19, 2021
0

Nyota kinda wa washika mitutu wa jiji...

Read more
Messi apata kadi Nyekundu ya kwanza kwa Barca

Messi apata kadi Nyekundu ya kwanza kwa Barca

Jan 18, 2021
Wateja wa Tigo Zanzibar kulipa bili za maji kwa Tigo Pesa

Wateja wa Tigo Zanzibar kulipa bili za maji kwa Tigo Pesa

Jan 14, 2021
Barcelona yahofia kumkosa Messi fainali za Supercopa de Espana

Barcelona yahofia kumkosa Messi fainali za Supercopa de Espana

Jan 14, 2021
Manchester United ipo tayari kuikabiri Liverpool – Pogba

Manchester United ipo tayari kuikabiri Liverpool – Pogba

Jan 13, 2021
Yanga waongeza Kitasa kutokea Mtibwa

Yanga waongeza Kitasa kutokea Mtibwa

Jan 11, 2021
Next Post
Vodacom Tanzania PLC yasherehekea na wateja kwenye maadhimisho ya wiki ya huduma kwa wateja

Vodacom Tanzania PLC yasherehekea na wateja kwenye maadhimisho ya wiki ya huduma kwa wateja

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

I agree to the Terms & Conditions and Privacy Policy.

Currently Playing

KRANTZ MWANTEPELE (FOUNDER & CEO)

ADVERTISEMENT

KONCEPT TV

https://www.youtube.com/watch?v=0HP0mB_rtIU&t=7s
ADVERTISEMENT
Mwanaharakati Mzalendo

Mwanaharakati Mzalendo ni mtandao namba moja kwa habari makini kutoka pande zote za dunia kuhusiana na Michezo, Siasa, Afya, Elimu, Mahusiano, Vituko, n.k

Wasiliana nasi kwa Email;krantzcharles@gmail.com
SIMU; 0658123310

Follow Us

October 2020
M T W T F S S
« Sep   Nov »
 1234
567891011
12131415161718
19202122232425
262728293031  
Currently Playing
  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

All rights reserved © 2020 Mwanaharakati Mzalendo - Powered by Koncept.

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv

All rights reserved © 2020 Mwanaharakati Mzalendo - Powered by Koncept.

Login to your account below

Forgotten Password?

Fill the forms bellow to register

*By registering into our website, you agree to the Terms & Conditions and Privacy Policy.
All fields are required. Log In

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In