Faida ya Benki ya NMB yapanda kwa asilimia 76 katika kipindi cha robo ya tatu ya mwaka 2020 – Mwanaharakati Mzalendo
ADVERTISEMENT
  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact
Mwanaharakati Mzalendo
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv
No Result
View All Result
Mwanaharakati Mzalendo
No Result
View All Result
Home BIASHARA

Faida ya Benki ya NMB yapanda kwa asilimia 76 katika kipindi cha robo ya tatu ya mwaka 2020

I am Krantz by I am Krantz
Oct 26, 2020
in BIASHARA
0 0
0
NMB yashinda tuzo ya benki salama zaidi nchini kwa mwaka 2020
0
SHARES
49
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Benki ya NMB imepata ongezeko la asilimia 76 la faida kabla ya kodi kwa kipindi kilichoishia Septemba 30, 2020.
Kwa miaka mitano sasa, Tanzania imeshuhudia ukuaji imara wa uchumi uliowezeshwa na sera thabiti za kiuchumi za Serikali ya awamu ya Tano. Maendeleo haya ya kiuchumi, mazingira rafiki ya kibiashara, pamoja na utekelezaji mzuri wa mikakati ya benki ya NMB ni sababu kuu zilizopelekea ongezeko hili la faida katika robo ya tatu ya mwaka 2020. Katika kipindi hiki faida kabla ya kodi ya Benki ya NMB imepanda kwa 76% kutoka Shilingi bilioni 118 katika robo ya tatu ya mwaka 2019 hadi shilingi bilioni 208 mwaka huu, wakati faida baada ya kodi ikipanda kutoka shilingi bilioni 82 hadi shilingi bilioni 145 ambayo ni sawa na ongezeko la 77%.
Pia katika kipindi hiki, mkakati wa Benki ya NMB wa kukuza vyanzo vya mapato umejidhihirisha kwa ongezeko la mapato yatokanayo na uendeshaji kwa 14% kutoka bilioni 527 katika robo ya tatu mwaka 2019 hadi bilioni 600 katika robo ya tatu ya mwaka huu (2020). Katika kipindi hiki pia programu za Benki za kudhibiti gharama za uendeshaji na matumizi ziliimarishwa na kusababisha uwiano mzuri wa gharama na mapato kwa 52%.

Vile vile, Benki ya NMB kama mwezeshaji mkubwa wa maendeleo na uchumi nchini, imeweza kukuza rasilimali zake kwa 15% kutoka shilingi trilioni 6.1 kipindi kama hiki mwaka jana hadi trilioni 7 katika robo ya tatu ya mwaka 2020; hili limesababishwa na ongezeko la amana za wateja kwa 15% na ongezeko la mikopo kwa wateja la 16%.

Benki yetu pia imepata mafanikio makubwa katika eneo la ukopeshaji kwa kupunguza tengo la mikopo chechefu kwa asilimia 22 ukilinganisha na kipindi husika mwaka 2019.

Kwa matokeo haya ya utekelezaji kwa kipindi hiki, Benki ya NMB imeendelea kuimarisha mtaji wake juu ya kiwango kilichowekwa kisheria na Benki Kuu ya Tanzania cha asilimia 12.5. Hiki ni kiashiria muhimu sana kuthibitisha afya ya Benki ya NMB kuendelea na biashara yake kwa miaka mingi ijayo.

ADVERTISEMENT

Akitangaza matokeo ya robo ya tatu ya mwaka 2020 ya Benki hiyo, Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB, Ruth Zaipuna alisema kuwa matokeo haya yamesababishwa na kukua kwa haraka kwa uchumi wa Tanzania, sera wezeshi na mwendelezo wa ukuaji wa pato la taifa kwa miaka ya hivi karibuni kama ilivyodhihirishwa kwa nchi yetu kuingia kwenye uchumi wa kati mwezi Julai mwaka 2020. Haya yote yamesababisha sekta ya kibenki kufanya vizuri, ikiwemo Benki ya NMB.

Bi. Zaipuna alisema kuwa “utendaji mzuri wa kifedha wa Benki ya NMB mwaka wote wa 2020 ni kielelezo kizuri cha ufanisi wa utekelezaji wa mikakati ya Benki, ubora wa wafanyakazi wetu na imani ya wateja wetu kuendelea kutumia huduma zetu za kibenki. Tunaendelea kuwashukuru wateja wetu, wanahisa wote na wafanyakazi wetu wote kwa matokeo haya chanya”.

Ni katika muktadha huo, wiki iliyopita, benki ya NMB ilipata tuzo ya Benki Salama zaidi Tanzania kwa mwaka 2020 itolewayo na jarida la kimataifa la Global Finance la New York, nchini Marekani. Ushindi huu umepatikana miezi kadhaa tangu jarida la Euromoney la London liitangaze Benki ya NMB kuwa Benki Bora Tanzania kwa miaka nane mfululizo.

Tags: NMB
ADVERTISEMENT
I am Krantz

I am Krantz

Related Posts

Tigo yazindua huduma ya ‘Lipa Kwa Simu’
BIASHARA

Tigo yazindua huduma ya ‘Lipa Kwa Simu’

by I am Krantz
Jan 19, 2021
0

Huduma hii ya malipo, sasa itafahamika kama...

Read more
PATA PATA NA TIGO YAKABIDHI MILIONI 10 KWA WASHINDI WAWILI

PATA PATA NA TIGO YAKABIDHI MILIONI 10 KWA WASHINDI WAWILI

Jan 12, 2021
Arise B.V (Arise) inamiliki 34.9% ya hisa zilizokuwa za Rabobank katika Benki ya NMB ya Tanzania.

Arise B.V (Arise) inamiliki 34.9% ya hisa zilizokuwa za Rabobank katika Benki ya NMB ya Tanzania.

Jan 8, 2021
Jumla ya Shilingi Milioni 20 Zimeshatolewa katika Promosheni ya kila wiki ya NMB MastaBATA

Jumla ya Shilingi Milioni 20 Zimeshatolewa katika Promosheni ya kila wiki ya NMB MastaBATA

Jan 5, 2021
Vodacom Tanzania PLC yatwaa Tuzo ya kwanza ya uandaaji bora wa taarifa za Fedha kwa mwaka 2019

Vodacom Tanzania PLC yatwaa Tuzo ya kwanza ya uandaaji bora wa taarifa za Fedha kwa mwaka 2019

Jan 5, 2021
Vodacom yatamatisha kampeni ya Shangwe Shangwena kwa kukabidhi gari Dodoma

Vodacom yatamatisha kampeni ya Shangwe Shangwena kwa kukabidhi gari Dodoma

Jan 4, 2021
Next Post
NI KAMPENI ZA FUNGA KAZI UCHAGUZI 2020/MASTAA SIMBA: KAZE ANATISHA, HEH, TENA……MAGAZETINI LEO JUMANNE TAREHE 27

NI KAMPENI ZA FUNGA KAZI UCHAGUZI 2020/MASTAA SIMBA: KAZE ANATISHA, HEH, TENA......MAGAZETINI LEO JUMANNE TAREHE 27

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

I agree to the Terms & Conditions and Privacy Policy.

Currently Playing

KRANTZ MWANTEPELE (FOUNDER & CEO)

ADVERTISEMENT

KONCEPT TV

https://www.youtube.com/watch?v=0HP0mB_rtIU&t=7s
ADVERTISEMENT
Mwanaharakati Mzalendo

Mwanaharakati Mzalendo ni mtandao namba moja kwa habari makini kutoka pande zote za dunia kuhusiana na Michezo, Siasa, Afya, Elimu, Mahusiano, Vituko, n.k

Wasiliana nasi kwa Email;krantzcharles@gmail.com
SIMU; 0658123310

Follow Us

October 2020
M T W T F S S
« Sep   Nov »
 1234
567891011
12131415161718
19202122232425
262728293031  
Currently Playing
  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

All rights reserved © 2020 Mwanaharakati Mzalendo - Powered by Koncept.

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv

All rights reserved © 2020 Mwanaharakati Mzalendo - Powered by Koncept.

Login to your account below

Forgotten Password?

Fill the forms bellow to register

*By registering into our website, you agree to the Terms & Conditions and Privacy Policy.
All fields are required. Log In

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In