APS YATOA MSAADA WA TAULO ZA KIKE ‘KIPEPEO PAD’ SHINYANGA – Mwanaharakati Mzalendo
ADVERTISEMENT
  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact
Mwanaharakati Mzalendo
ADVERTISEMENT
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv
No Result
View All Result
Mwanaharakati Mzalendo
No Result
View All Result
Home BIASHARA

APS YATOA MSAADA WA TAULO ZA KIKE ‘KIPEPEO PAD’ SHINYANGA

I am Krantz by I am Krantz
Nov 3, 2020
in BIASHARA
0 0
0
APS YATOA MSAADA WA TAULO ZA KIKE ‘KIPEPEO PAD’ SHINYANGA
0
SHARES
75
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga, Mhe. Jasinta Mboneko akionesha taulo za kike ‘Kipepeo Pad’ zilizotolewa na Kampuni ya APS (Aspire Products & Services Co. Ltd), kwa ajili ya wanafunzi wanaosoma katika shule ya Msingi Ushirika iliyopo katika kata ya Chamaguha Manispaa ya Shinyanga. Kulia ni Mkurugenzi wa Kampuni ya APS, Janeth Dutu. Picha zote na Kadama Malunde – Malunde 1 blog
Kulia ni Mkurugenzi wa Kampuni ya APS  Janeth Dutu akimkabidhi Taulo za kike ‘Kipepeo Pad’ Mkuu wa wilaya ya Shinyanga, Mhe. Jasinta Mboneko kwa ajili ya wanafunzi wanaosoma katika shule ya Sekondari Chamaguha na shule ya Msingi Ushirika.
Muonekano wa sehemu ya taulo za kike ‘Kipepeo Pad’ kwa ajili ya wanafunzi wanaosoma katika shule ya Msingi Ushirika na shule ya sekondari Chamaguha zilizotolewa  Kampuni ya APS.
Muonekano wa sehemu ya maboksi yenye taulo za kike ‘Kipepeo Pad’ kwa ajili ya wanafunzi wanaosoma katika shule ya Msingi Ushirika na shule ya sekondari Chamaguha zilizotolewa  Kampuni ya APS.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga, Mhe. Jasinta Mboneko akigawa taulo za kike ‘Kipepeo Pad’ kwa mwanafunzi anayesoma katika shule ya Msingi Ushirika.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga, Mhe. Jasinta Mboneko akigawa taulo za kike ‘Kipepeo Pad’ kwa mwanafunzi anayesoma katika shule ya Msingi Ushirika.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga, Mhe. Jasinta Mboneko akizungumza wakati akigawa taulo za kike ‘Kipepeo Pad’ kwa mwanafunzi wanaosoma katika shule ya Msingi Ushirika. Kushoto ni Afisa Mtendaji Kata ya Chamaguha, Irene Mshandete. Kulia ni Mkurugenzi wa Kampuni ya APS, Janeth Dutu.
Mkurugenzi wa Kampuni ya APS (Aspire Products & Services Co. Ltd), Janeth Dutu akielezea lengo la kutoa taulo za kike kwa wanafunzi wa kike katika shule ya msingi Ushirika na shule ya sekondari Chamaguha kuwa ni kusaidia kupunguza utoro shuleni kwani baadhi ya wanafunzi wa kike wamekuwa hawaendi shuleni kutokana na kukosa taulo za kike wanapokuwa katika hedhi.
Waliowahi kuwa wanafunzi wa shule ya msingi Ushirika walioambatana na Mkurugenzi wa Kampuni ya APS (Aspire Products & Services Co. Ltd), Janeth Dutu kutoa taulo za kike kwa wanafunzi wa kike katika shule ya msingi Ushirika wakiwa wamekaa. Wa kwanza kushoto ni Zubery Bundala akifuatiwa na Agnes Mambosasa, Eva Laurent na Sara Elias.
Mkurugenzi wa Kampuni ya APS (Aspire Products & Services Co. Ltd), Janeth Dutu na Sara Elias wakipiga picha na wanafunzi wa shule ya msingi Ushirika.
Mkurugenzi wa Kampuni ya APS (Aspire Products & Services Co. Ltd), Janeth Dutu na waliowahi kuwa wanafunzi wa shule ya msingi Ushirika wakipiga picha ya kumbukumbu na wanafunzi na mmoja wa walimu wa muda mrefu wa shule hiyo baada ya kutoa taulo za kike.
Kushoto ni Mkurugenzi wa Kampuni ya APS (Aspire Products & Services Co. Ltd), Janeth Dutu akimkabidhi Taulo za kike ‘Kipepeo Pad’ Mkuu wa wilaya ya Shinyanga, Mhe. Jasinta Mboneko kwa ajili ya wanafunzi wanaosoma katika shule ya Sekondari Chamaguha iliyopo katika kata ya Chamaguha Manispaa ya Shinyanga leo Jumatatu Novemba 2,2020 katika shule ya Sekondari Chamaguha.
Mkurugenzi wa Kampuni ya APS (Aspire Products & Services Co. Ltd), Janeth Dutu akionesha na kuwaelezea wanafunzi na walimu wa shule ya Sekondari Chamaguha namna taulo za kike ‘Kipepeo Pad’ zilivyo bora.
Mkurugenzi wa Kampuni ya APS (Aspire Products & Services Co. Ltd), Janeth Dutu akiwaonesha wanafunzi wa shule ya Sekondari Chamaguha namna taulo za kike ‘Kipepeo Pad’ zilivyo bora.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga, Mhe. Jasinta Mboneko akizungumza wakati akigawa taulo za kike ‘Kipepeo Pad’ kwa mwanafunzi wanaosoma katika shule ya Sekondari Chamaguha.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga, Mhe. Jasinta Mboneko akigawa taulo za kike ‘Kipepeo Pad’ kwa mwanafunzi anayesoma katika shule ya Sekondari Chamaguha. Wa kwanza kulia ni Mkurugenzi wa Kampuni ya APS, Janeth Dutu.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga, Mhe. Jasinta Mboneko akigawa taulo za kike ‘Kipepeo Pad’ kwa mwanafunzi anayesoma katika shule ya Sekondari Chamaguha. Wa kwanza kulia ni Mkurugenzi wa Kampuni ya APS, Janeth Dutu.
Elizabeth Kagongoo kutoka shule ya sekondari Chamaguha akiishukuru Kampuni ya APS kwa kuwapatia taulo za kike.
Wanafunzi wa shule ya sekondari Chamaguha wakionesha Taulo za kike ‘Kipepeo Pad’
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga, Mhe. Jasinta Mboneko, Mkurugenzi wa Kampuni ya APS, Viongozi wa kata ya Chamaguha, Manispaa ya Shinyanga, walimu na wanafunzi wa shule ya sekondari Chamaguha wakipiga picha ya kumbukumbu.
Mkurugenzi wa Kampuni ya APS, Janeth Dutu akipiga picha na wanafunzi wa shule ya sekondari Chamaguha.
Mkurugenzi wa Kampuni ya APS  Janeth Dutu akiagana na Mkuu wa wilaya ya Shinyanga, Mhe. Jasinta Mboneko (kulia) baada ya zoezi la kugawa Taulo za kike ‘Kipepeo Pad’ kwa ajili ya wanafunzi wanaosoma katika shule ya Sekondari Chamaguha na shule ya Msingi Ushirika.
 
Na Kadama Malunde – Malunde 1 blog
Kampuni ya Aspire Products & Services Co. Ltd (APS Company)  inayojihusisha na utengenezaji na usambazaji  wa Taulo za kike  maarufu kwa jina Kipepeo Pad imetoa msaada wa taulo za kike 400 kwa wanafunzi 30 wanaosoma katika shule ya msingi Ushirika na shule ya Sekondari Chamaguha zilizopo katika kata ya Chamaguha Manispaa ya Shinyanga.
Hafla fupi ya makabidhiano ya Taulo  za kike ‘Pedi’ imefanyika leo katika shule ya Ushirika na Chamaguha na kuhudhuriwa na Mkurugenzi wa Kampuni ya APS Janeth Dutu aliyeambatana na baadhi ya waliokuwa  wanafunzi wa shule ya msingi Ushirika ambapo mgeni rasmi alikuwa mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko.
Akizungumza wakati wa kupokea Taulo hizo za kike kutoka Kampuni ya APS, Mkuu wa wilaya ya Shinyanga, Mhe. Jasinta Mboneko aliishukuru Kampuni ya APS kwa msaada huo akibainisha kuwa zitasaidia kupunguza utoro kwa wanafunzi wa kike  wanapokuwa katika hedhi.
“Asanteni sana APS Company kwa msaada wa taulo za kike kwa ajili ya wanafunzi 10 wanaosoma katika shule ya msingi Ushirika na wanafunzi 20 wanaosoma katika shule ya sekondari Chamaguha watakazozitumia kwa muda wa mwaka mmoja. Hakika mmeunga mkono kwa vitendo kampeni yetu ya  ‘Msitiri msichana,punguza utoro shuleni’ tuliyoianzisha hivi karibuni”,amesema Mboneko.
“Tunakushukuru ndugu yetu Janeth Dutu kupitia Kampuni yako ya APS pamoja na waliowahi kuwa wanafunzi wa shule ya msingi Ushirika ambao umeambatana nao leo kuleta taulo za kike. Hii ni sadaka kubwa mmetoa”,ameongeza Mboneko.
Mkuu huyo wa wilaya ametumia fursa hiyo kuwaomba wadau wengine kujitokeza kusaidia upatikanaji wa taulo za kike shuleni kwani bado wanafunzi wa kike wanapata changamoto akieleza kuwa lengo la serikali ni kuhakikisha wanafunzi wanasoma katika mazingira rafiki.
Katika hatua nyingine Mboneko amewataka wanafunzi kusoma kwa bidii na kuepuka vikundi viovu na vishawishi mbalimbali vinavyoweza kukatisha ndoto zao.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Kampuni ya Aspire Products & Services Co. Ltd (APS), Janeth Dutu amesema lengo la kutoa taulo za kike ni kupunguza utoro shuleni kwani baadhi ya wanafunzi wa kike wamekuwa hawaendi shuleni kutokana na kukosa taulo za kike wanapokuwa katika hedhi.
Amesema kutokana na uwepo wa taulo za kike wanafunzi watahudhuria masomo yao hata kama wapo katika hedhi hivyo ufaulu wao utaongezeka.
“Ninaamini kabisa taulo zetu za kike zinazojulikana kwa jina la Kipepeo Pad ambazo zina ubora wa hali ya juu zitawasaidia wanafunzi 10 katika shule ya msingi Ushirika ambayo nilisoma lakini pia wanafunzi 20 katika shule ya sekondari Chamaguha ambapo nitaendelea kuwahudumia wanafunzi hawa kwa muda wa mwaka mmoja”,amesema Janeth.
Akizungumza  kwa niaba ya wanafunzi walionufaika na msaada huo, Elizabeth Kagongoo kutoka shule ya sekondari Chamaguha ameishukuru Kampuni ya APS kwa kuwapatia taulo za kike akieleza kuwa awali walikuwa wanalazimik kutumia vitambaa na wakati mwingine baadhi yao kuwa watoro shuleni pindi wanapokuwa katika hedhi.
I am Krantz

I am Krantz

Related Posts

NMB yazindua Bima ya simu za mkononi
BIASHARA

NMB yazindua Bima ya simu za mkononi

by I am Krantz
Apr 19, 2021
0

 Afisa Mkuu wa Wateja Binafsi na Biashara wa NMB, Filbert Mponzi(kulia) na...

Read more
Tigo yaungana na TAPSOA kuwezesha wateja kufanya malipo ya mafuta kwa Tigo Pesa

Tigo yaungana na TAPSOA kuwezesha wateja kufanya malipo ya mafuta kwa Tigo Pesa

Apr 16, 2021
Mawakala wa Tigo Pesa washinda mamilioni

Mawakala wa Tigo Pesa washinda mamilioni

Apr 15, 2021
Zantel yazindua ofa ya mfungo wa Ramadhan

Zantel yazindua ofa ya mfungo wa Ramadhan

Apr 15, 2021
Vodacom yashirikiana na Britam Tanzania kuzindua VodaBima kupitia M-Pesa

Vodacom yashirikiana na Britam Tanzania kuzindua VodaBima kupitia M-Pesa

Apr 13, 2021
Bolt yazindua Web App kupanua huduma za usafiri Tanzania

Bolt yapokea uwekezaji wa Euro 20 milioni kutoka IFC

Apr 11, 2021
Next Post
Akamatwa na Polisi kwa tuhuma za kutoa mimba na kumsababisha kifo

Akamatwa na Polisi kwa tuhuma za kutoa mimba na kumsababisha kifo

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

I agree to the Terms & Conditions and Privacy Policy.

Currently Playing

KRANTZ MWANTEPELE (FOUNDER & CEO)

ADVERTISEMENT

KONCEPT TV

https://www.youtube.com/watch?v=0HP0mB_rtIU&t=7s
Mwanaharakati Mzalendo

Mwanaharakati Mzalendo ni mtandao namba moja kwa habari makini kutoka pande zote za dunia kuhusiana na Michezo, Siasa, Afya, Elimu, Mahusiano, Vituko, n.k

Wasiliana nasi kwa Email;krantzcharles@gmail.com
SIMU; 0658123310

Follow Us

November 2020
M T W T F S S
« Oct   Dec »
 1
2345678
9101112131415
16171819202122
23242526272829
30  
Currently Playing
  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

All rights reserved © 2020 Mwanaharakati Mzalendo - Powered by Koncept.

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv

All rights reserved © 2020 Mwanaharakati Mzalendo - Powered by Koncept.

Login to your account below

Forgotten Password?

Fill the forms bellow to register

*By registering into our website, you agree to the Terms & Conditions and Privacy Policy.
All fields are required. Log In

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In