Benki ya NMB imetoa misaada kwa Wilaya ya Kilwa mkoani Lindi katika sekta ya afya na elimu yenye jumla ya shilingi milioni 12.5 – Mwanaharakati Mzalendo
ADVERTISEMENT
  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact
Mwanaharakati Mzalendo
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv
No Result
View All Result
Mwanaharakati Mzalendo
No Result
View All Result
Home HABARI

Benki ya NMB imetoa misaada kwa Wilaya ya Kilwa mkoani Lindi katika sekta ya afya na elimu yenye jumla ya shilingi milioni 12.5

I am Krantz by I am Krantz
Nov 24, 2020
in HABARI
0 0
0
Benki ya NMB imetoa misaada kwa Wilaya ya Kilwa mkoani Lindi katika sekta ya afya na elimu yenye jumla ya shilingi milioni 12.5
0
SHARES
38
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

 




Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa – Renatus Mchau akipokea msaada wa madawati 100 kutoka kwa Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Kusini – Janeth Shango .Katikati ni Nelly Masisi – Meneja wa NMB Tawi la Kilwa. Hafla hiyo ilihudhuriwa na wazazi pamoja na  wanafunzi wa Shule hiyo .


Benki ya NMB imetoa misaada kwa Wilaya ya Kilwa mkoani Lindi katika sekta ya afya na elimu yenye jumla ya shilingi milioni 12.5 


Akikabidhi misaada hiyo kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa – Renatus Mchauru, Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Kusini – Janeth Shango, alisema wakati anapata matibabu katika kituo cha afya Masoko, alibaini mapugufu yaliyokuwepo katika kituo hicho na alipozungumza na utawala walimweleza tatizo na akawashauri waandike barua ya kujieleza, kitu ambacho walifanya.

 

Alisema Benki ya NMB imekarabati jengo la Baba, Mama na Mtoto kwa kuweka paa jipya, kupaka rangi na kuweka michoro ambayo inaleta taswira njema kwa wadau wanaofuata tiba. Alisema Benki hiyo inaona fahari kusaidia eneo hilo ili liwe rafiki kwa wahitaji.Alisema kazi ya kukarabati jengo hilo la hospitali katika kituo cha afya Masoko uligharimu Sh milioni 2.5.

 

Naye Mganga Mfawidhi wa kituo hicho, John Nkuba alishukuru Benki ya NMB kwa msaada wake na kusema kwamba mazingira ya matibabu sasa baada ya ukarabati huo yako bora zaidi.

 

Mkurugenzi wa Wilaya ya Kilwa- Renatus Mchauru pamoja na kushukuru kwa misaada hiyo, aliwataka watumishi kuhakikisha wanatoa huduma nzuri na bora zaidi kulingana na uzuri wa majengo yaliyopo sasa.

 

Akizungumza wakati wa kukabidhi madawati katika shule ya msingi ya Msingi Kipindimbi, Shango alisema wametoa madawati 100 kwa ajili ya wanafunzi wapya wa shule hiyo.

 

Shule hiyo iliyokuwa na madawati 100 ilizidiwa baada ya wanafunzi kuongezeka kufuatia maafa ya mafuriko  yaliyokumba shule na makazi katika kata ya Njinjo mwanzoni mwa mwaka huu. Shule hizo ni pamoja na Njinjo na Ndende.

 

Maafa hayo yaliyokumba watu zaidi ya 6,804 katika kata ya Njinjo yalisababisha Shule ya Kipindimbi  wanafunzi wake kuongezeka kutoka watoto 400 hadi 909 na kusababisha upungufu wa madawati zaidi ya 100.

 

Katika hafla zote mbili Shango alishauri wazazi kuanza mapema kuwafunza watoto wao kuweka akiba kwa kuwafungulia akaunti watoto wao ili waweze kuja kujisaidia siku za baadae.

 

ADVERTISEMENT

Mwalimu Mkuu wa shule hiyo,Bahati alisema pamoja na kusaidiwa madawati hayo , shule hiyo bado inakabiliwa na tatizo la matundu ya choo kwa wanafunzi na walimu na  pia nyumba za walimu.

 

Wanafunzi wa shule hiyo Khalid Salim na Neema Ali waliishukuru Benki ya NMB kwa kuwasaidia madawati hayo na kuwataka wawasaidie pia matundu ya choo. 


ADVERTISEMENT
I am Krantz

I am Krantz

Related Posts

IGP Sirro akemea vitendo vya udhalilishaji Zanzibar
HABARI

IGP Sirro akemea vitendo vya udhalilishaji Zanzibar

by Mhariri
Jan 22, 2021
0

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP...

Read more
Kiwanda cha Twiga Cement wamkabidhi RC Kunenge mifuko 800 ya Saruji

Kiwanda cha Twiga Cement wamkabidhi RC Kunenge mifuko 800 ya Saruji

Jan 22, 2021
Naibu Waziri Kipanga aagiza Vyuo vya VETA kwenye Wilaya 25 vyote vikamilike kwa wakati

Naibu Waziri Kipanga aagiza Vyuo vya VETA kwenye Wilaya 25 vyote vikamilike kwa wakati

Jan 22, 2021
Wakurugenzi watakiwa kujitathimini Ukusanyaji wa Mapato (+video)

Wakurugenzi watakiwa kujitathimini Ukusanyaji wa Mapato (+video)

Jan 22, 2021
Rais wa Zanzibar akutana na IGP Sirro

Rais wa Zanzibar akutana na IGP Sirro

Jan 22, 2021
Waziri Aweso awaagiza SUMAJKT kuongeza nguvu kazi kwenye ujenzi wa tanki la Maji Chamwino

Waziri Aweso awaagiza SUMAJKT kuongeza nguvu kazi kwenye ujenzi wa tanki la Maji Chamwino

Jan 22, 2021
Next Post
Video: Halima Mdee na wenzake waapishwa kuwa Wabunge viti maalum

Video: Halima Mdee na wenzake waapishwa kuwa Wabunge viti maalum

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

I agree to the Terms & Conditions and Privacy Policy.

Currently Playing

KRANTZ MWANTEPELE (FOUNDER & CEO)

ADVERTISEMENT

KONCEPT TV

https://www.youtube.com/watch?v=0HP0mB_rtIU&t=7s
ADVERTISEMENT
Mwanaharakati Mzalendo

Mwanaharakati Mzalendo ni mtandao namba moja kwa habari makini kutoka pande zote za dunia kuhusiana na Michezo, Siasa, Afya, Elimu, Mahusiano, Vituko, n.k

Wasiliana nasi kwa Email;krantzcharles@gmail.com
SIMU; 0658123310

Follow Us

November 2020
M T W T F S S
« Oct   Dec »
 1
2345678
9101112131415
16171819202122
23242526272829
30  
Currently Playing
  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

All rights reserved © 2020 Mwanaharakati Mzalendo - Powered by Koncept.

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv

All rights reserved © 2020 Mwanaharakati Mzalendo - Powered by Koncept.

Login to your account below

Forgotten Password?

Fill the forms bellow to register

*By registering into our website, you agree to the Terms & Conditions and Privacy Policy.
All fields are required. Log In

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In