Halmashauri 45 zapewa siku tano kutoa maelezo ya kutoanzisha kamati za wenye ulemavu – Mwanaharakati Mzalendo
ADVERTISEMENT
  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact
Mwanaharakati Mzalendo
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv
No Result
View All Result
Mwanaharakati Mzalendo
No Result
View All Result
Home HABARI

Halmashauri 45 zapewa siku tano kutoa maelezo ya kutoanzisha kamati za wenye ulemavu

Mhariri by Mhariri
Nov 27, 2020
in HABARI
0 0
0
Halmashauri 45 zapewa siku tano kutoa maelezo ya kutoanzisha kamati za wenye ulemavu
0
SHARES
42
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na Angela Msimbira OR-TAMISEMI

Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa anayeshughulikia afya Dkt. Dorothy Gwajima amezitaka Halmashauri 45 ambazo hazijaunda kamati za watu wenye ulemavu kutoa maelezo ndani ya siku tano.

Akifungua Mkutano wa wadau wa Chama cha Wazazi wenye watoto wenye vichwa vikubwa na migongo wazi leo amesema hadi sasa halmashauri 140 zimeunda kamati hizo lakini nyingine bado hazijafanya hivyo, jambo ambalo linarudisha nyuma mikakati ya Serikali ya kuwasaidia watu wenye ulemavu.

Amesema kamati hizo ni muhimu kuundwa kwa kuwa zinarahisha mawasiliano kati ya jamii ya watu wenye ulemavu na serikali na kuweka mikakati bora ya jinsi ya kutatua changamoto zao wanazozipitia katika jamii kwa haraka.

“Kwa halmashauri ambazo hazijaunda kamati hizo natoa siku tano kutoa maelezo wanataka nini ili waunde kamati hizo,waliambiwa mwaka gani na sababu za kutokuunda kamati ni nini na wana mikakati gani ya kuanzisha kamati hizo”, ameagiza Dkt. Gwajima.

Hata hivyo Dkt. Gwajima amesema kuwa kutokuundwa kwa kamati hizo kumesababisha kukata mawasiliano kati ya jamii ya watu wenye ulemavu na Serikali katika suala zima la utoaji wa huduma za afya kwa jamii kwa kuwa lengo la serikali ni kuwafikia watu wenye uhitaji.

ADVERTISEMENT

Aidha Dkt. Gwajima amewataka wadau mbalimbali nchini kuhakikisha wanatoa elimu kwa jamii kuhusu umuhimu wa lishe bora kabla ya Ujauzito ili kupunguza tatizo la watoto wenye mgongo wazi na vichwa vikubwa nchini.

Dkt. Gwajima amesema kuwa kuna umuhimu wa kuweka mikakati itakayosaidia kutoa elimu kuanzia ngazi ya chini ili kujenga uelewa wa pamoja kuhusu umuhimu wa lishe bora kwa jamii, jambo ambalo litasaidia kumaliza au kupumguza kabisa tatizo la kupata watoto wenye vichwa vikubwa na migongo wazi.

Dkt. Gwajima amesema Serikali imeendelea kuweka mikakati ya kuboresha huduma kwa kujenga na kukarabati vituo vya afya nchini na kupeleka vifaa tiba kwa lengo la kuhakikisha huduma bora za afya zinatolewa kwa wananchi.

Hivyo Dkt.Gwajima ametoa wito kwa wananchi kuhakikisha wanatumia vituo vya afya hasa kwa wale watoto wenye matatizo ya mgongo wazi na vichwa vikubwa.

Pia ameitaka jamii kuacha mila potofu za kuamini kuwa mtoto anapozaliwa na tatizo la Mgongo wazi na kichwa kikubwa kuwa wamelogwa hivyo kupelekea baadhi ya wazazi kuwaficha watoto wao jambo ambalo linasababisha ucheleweshwa kwa matibabu ambayo yangemsaidia kupona kwa haraka.

“Jamii ielimishwe kuhusu chanzo cha kuzaliwa kwa watoto wenye migongo wazi na vichwa vikubwa ili waondokane na dhana potofu walizonazo ili kuwaokoa watoto wenye tatizo hilo na jinsi ya kukabiliana nalo” amesisitiza Dkt. Gwajima.

Dkt. Gwajima ameagiza wadau wote kuhakikisha wanatoa elimu kwa kamati za vituo vya afya nchini kwa kuwa zina wananchi ambao ni wajumbe ili wajue takwimu sahihi ya watoto wenye vichwa vikubwa.

“Wekeni mikakati ya kutumia mifumo ya afya iliyopo katika jamii ili kupunguza watoto wenye vichwa vikubwa na mgongo wazi katika jamii yetu”, ameeleza Dkt. Gwajima.

ADVERTISEMENT
Mhariri

Mhariri

Related Posts

Binti achanganyikiwa baada ya mchumba kutoweka siku chache kabla ya ndoa, apata ufumbuzi
HABARI

Binti achanganyikiwa baada ya mchumba kutoweka siku chache kabla ya ndoa, apata ufumbuzi

by Mhariri
Jan 18, 2021
0

Kwa majina naitwa Aisha Hamisi, umri wa...

Read more
Serikali yapiga marufuku ulaji wa nyama ya Nguruwe

Serikali yapiga marufuku ulaji wa nyama ya Nguruwe

Jan 18, 2021
Naibu Waziri Kipanga aiagiza kamati ya Ujenzi VETA Korogwe kukamilisha ujenzi huo kwa wakati

Naibu Waziri Kipanga aiagiza kamati ya Ujenzi VETA Korogwe kukamilisha ujenzi huo kwa wakati

Jan 18, 2021
Mashirika ya Umma yenye malimbikizo ya madeni TTCL kukatiwa huduma Januari 31

Mashirika ya Umma yenye malimbikizo ya madeni TTCL kukatiwa huduma Januari 31

Jan 18, 2021
Bodi ya maziwa yaiweka kikaangoni kampuni ya maziwa ya Cowbell

Bodi ya maziwa yaiweka kikaangoni kampuni ya maziwa ya Cowbell

Jan 18, 2021
Hospitali ya Uhuru yaanza kutoa Huduma

Hospitali ya Uhuru yaanza kutoa Huduma

Jan 17, 2021
Next Post
Tigo yaendelea kukabidhi zawadi za Simu kwa washindi mbalimbali wa #JazaTukujazeTena

Tigo yaendelea kukabidhi zawadi za Simu kwa washindi mbalimbali wa #JazaTukujazeTena

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

I agree to the Terms & Conditions and Privacy Policy.

Currently Playing

KRANTZ MWANTEPELE (FOUNDER & CEO)

ADVERTISEMENT

KONCEPT TV

https://www.youtube.com/watch?v=0HP0mB_rtIU&t=7s
ADVERTISEMENT
Mwanaharakati Mzalendo

Mwanaharakati Mzalendo ni mtandao namba moja kwa habari makini kutoka pande zote za dunia kuhusiana na Michezo, Siasa, Afya, Elimu, Mahusiano, Vituko, n.k

Wasiliana nasi kwa Email;krantzcharles@gmail.com
SIMU; 0658123310

Follow Us

November 2020
M T W T F S S
« Oct   Dec »
 1
2345678
9101112131415
16171819202122
23242526272829
30  
Currently Playing
  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

All rights reserved © 2020 Mwanaharakati Mzalendo - Powered by Koncept.

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv

All rights reserved © 2020 Mwanaharakati Mzalendo - Powered by Koncept.

Login to your account below

Forgotten Password?

Fill the forms bellow to register

*By registering into our website, you agree to the Terms & Conditions and Privacy Policy.
All fields are required. Log In

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In