Mradi wa majaribio wa kilimo cha mtama wa TBL Plc , FtMA, WFP wanufaisha wakulima 1,300 nchini – Mwanaharakati Mzalendo
ADVERTISEMENT
  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact
Mwanaharakati Mzalendo
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv
No Result
View All Result
Mwanaharakati Mzalendo
No Result
View All Result
Home BIASHARA

Mradi wa majaribio wa kilimo cha mtama wa TBL Plc , FtMA, WFP wanufaisha wakulima 1,300 nchini

I am Krantz by I am Krantz
Nov 22, 2020
in BIASHARA, HABARI
0 0
0
Mradi wa majaribio wa kilimo cha mtama wa TBL Plc , FtMA, WFP wanufaisha wakulima 1,300 nchini
0
SHARES
62
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter
ADVERTISEMENT


Mmoja wa wakulima wa zao la Mtama katika eneo la Kibaigwa wilaya ya Kongwa mkoani Dodoma,Sebastian Msola (Kulia) akitoa maelezo kwa ujumbe kutoka TBL , WFP na FtMA walipofika kumtembelea shambani kwake mwishoni mwa wiki wakati wa tathmini ya mradi wa pamoja wa kuwezesha wakulima wa zao hilo katika mikoa ya Dodoma na Manyara


 

Baadhi ya wakulima wa mtama wanawake katika mkutano wa tathmini

Bi Hilda Madeje, mkulima wa mtama katika kijiji cha Sagala B kilichopo wilayani Kongwa mkoani Dodoma.sasa ana soko la uhakika la kuuzia magunia 30 ya mtama ambayo ni ongezeko la 70% kulinganisha na miaka ya nyuma.Hali hii imemuwezesha kupata fedha za kutosha kujenga nyumba ya kuishi familia yake na kulipia ada ya shule kwa watoto wake  4.
Bi Madeje ni mmoja wa washiriki wa mradi wa majaribio wa kilimo cha mtama  wa kampuni ya bia  ya TBL Plc, taasisi ya Farm to Market Alliance(FtMA) na Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP), ambao ulilenga kuwawezesha wakulima wa mtama  mbinu za kisasa za kulima zao hilo kwa kuwapatia mbegu bora za mtama na kuongeza mavuno sambamba na kuwahakikishia soko la uhakika la mavuno yao.
Mradi huu wa ushirikiano ulianza mwezi Januari 2020 ambapo kampuni ya TBL Plc ilikubali kununua mtama unaozalishwa na wakulima mkoani Dodoma, TBL Plc, FtMa na WFP iliwasaidia wakulima hao kupata mbegu ya mtama; bima ya mazao; itifaki za usimamizi wa zao la mtama; huduma za ugani za kilimo; pamoja na ujumuishaji bora na soko la uhakika ili waweze kuongeza mavuno yao.
Akizungumza wakati wa tathmini ya msimu uliopita iliyofanyika mkoani Dodoma wiki iliyopita, Meneja Kilimo wa TBL Plc, Joel Msechu, alisema kuwa TBL Plc ililipa wakulima wadogo jumla ya Tzs 1.75 bilioni kwa ajili ya kununua tani 3,000 za mtama uliozalishwa katika wilaya za  Mpwapwa, Kongwa, Kondoa,  Bahi na Chamwino mkoani Dodoma, ambapo kila kilo ya mtama ilinunuliwa kwa shilingi 550. “Mradi umekuwa na matokeo mazuri na umewezesha  kuboresha maisha ya wakulima wa mtama” aliongeza.
Kwa mujibu wa Msechu kampuni kwa sasa inanunua asilimia 74% ya malighafi zake nchini na imedhamiria kuongeza kiwango cha ununuzi wa malighafi nchini katika  miaka ijayo.TBL Plc imejipanga kuhakikisha inashirikiana na wakulima wa mtama wapatao 6,000 katika  msimu wa 2020-2021 ili kukidhi kupata mahitaji yake ya tani 10,000 za mtama kwa ajili za kuzalisha chapa zake za Eagle na Bingwa.
Akiongea katika mkutano huo wa tathmini,Mwakilishi wa WFP, Lusajo Bukuku alisema kabla ya kuanzishwa kwa mradi huo wakulima walikuwa wanazalisha magunia 3 hadi 4 ya mtama kwa ekari.Kutokana na kupatiwa mbinu bora za kilimo na usimamizi mzuri mavuno yao kwa sasa yameongezeka kufikia karibu magunia kati ya 10 hadi 11 kwa ekari.
Naye Mwakilishi wa Farm Africa ,William Mwakyami,alisema kupitia mradi huu,taasisi yao imesaidia kuwezesha wakulima wapatao 846 ambao wamenufaika kwa kujiongezea kipato kutokana na kuzalisha zaidi kulinganisha na kipindi cha nyuma kabla ya mradi na wameweza kuwa na soko la uhakika la mavuno yao.
 
Kaimu Afisa Kilimo wa Wilaya ya Kongwa, Bi Amina Msangi, amesema kabla ya kuanzishwa kwa mradi huu wakulima walikuwa wanakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ukosefu wa soko la uhakika la mavuno yao. Alitoa wito kwa wakulima kuchangamkia  fursa hii ya soko la uhakika iliyopatikana ili iwasaidie kujikwamua kimaisha.
Mpango wa  TBL Plc wa kununua malighafi nchini ni moja ya mchango wa kampuni ambao unaenda sambamba kufanikisha jitihada za Serikali katika kukuza uchumi wa Tanzania.

Mwaka 2018, ABInBev ilijitoa kuwapatia ujuzi, kuwaunganisha na kuwawezesha kifedha wakulima mpaka kufikia mwaka 2025. Kutokana na mkakati huo,TBL Plc  imefanya uwekezaji wenye lengo la kuwainua wakulima wadogo nchini Tanzania kwa kuwaanzishia huduma mbalimbali-Kilimo Uza. Kutumiwa meseji za simu kuwapatia taarifa mbalimbali kama hali ya hewa, taarifa za masoko, ushauri wa kitaalamu. huduma ya mkopo wa pembejeo, mafunzo kuhusiana na masuala ya fedha na ununuzi wa pembejeo bora na matumizi yake, matokeo ya utafiti wa mbegu bora za mtama unaofaa kuzalishwa nchini, mbinu za kilimo cha kisasa sambamba na kuwasaidia katika kipindi chote cha msimu wa kilimo ili waweze kusimama na kufanya vizuri zaidi.

Tags: TBL
ADVERTISEMENT
I am Krantz

I am Krantz

Related Posts

Binti achanganyikiwa baada ya mchumba kutoweka siku chache kabla ya ndoa, apata ufumbuzi
HABARI

Binti achanganyikiwa baada ya mchumba kutoweka siku chache kabla ya ndoa, apata ufumbuzi

by Mhariri
Jan 18, 2021
0

Kwa majina naitwa Aisha Hamisi, umri wa...

Read more
Serikali yapiga marufuku ulaji wa nyama ya Nguruwe

Serikali yapiga marufuku ulaji wa nyama ya Nguruwe

Jan 18, 2021
Naibu Waziri Kipanga aiagiza kamati ya Ujenzi VETA Korogwe kukamilisha ujenzi huo kwa wakati

Naibu Waziri Kipanga aiagiza kamati ya Ujenzi VETA Korogwe kukamilisha ujenzi huo kwa wakati

Jan 18, 2021
Mashirika ya Umma yenye malimbikizo ya madeni TTCL kukatiwa huduma Januari 31

Mashirika ya Umma yenye malimbikizo ya madeni TTCL kukatiwa huduma Januari 31

Jan 18, 2021
Bodi ya maziwa yaiweka kikaangoni kampuni ya maziwa ya Cowbell

Bodi ya maziwa yaiweka kikaangoni kampuni ya maziwa ya Cowbell

Jan 18, 2021
Hospitali ya Uhuru yaanza kutoa Huduma

Hospitali ya Uhuru yaanza kutoa Huduma

Jan 17, 2021
Next Post
RC Kunenge awaelekeza wakazi wa Kunduchi Mtongani kuhama kuepuka volcano ya tope

RC Kunenge awaelekeza wakazi wa Kunduchi Mtongani kuhama kuepuka volcano ya tope

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

I agree to the Terms & Conditions and Privacy Policy.

Currently Playing

KRANTZ MWANTEPELE (FOUNDER & CEO)

ADVERTISEMENT

KONCEPT TV

https://www.youtube.com/watch?v=0HP0mB_rtIU&t=7s
ADVERTISEMENT
Mwanaharakati Mzalendo

Mwanaharakati Mzalendo ni mtandao namba moja kwa habari makini kutoka pande zote za dunia kuhusiana na Michezo, Siasa, Afya, Elimu, Mahusiano, Vituko, n.k

Wasiliana nasi kwa Email;krantzcharles@gmail.com
SIMU; 0658123310

Follow Us

November 2020
M T W T F S S
« Oct   Dec »
 1
2345678
9101112131415
16171819202122
23242526272829
30  
Currently Playing
  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

All rights reserved © 2020 Mwanaharakati Mzalendo - Powered by Koncept.

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv

All rights reserved © 2020 Mwanaharakati Mzalendo - Powered by Koncept.

Login to your account below

Forgotten Password?

Fill the forms bellow to register

*By registering into our website, you agree to the Terms & Conditions and Privacy Policy.
All fields are required. Log In

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In