NBC yazindua akaunti ya ‘NBC Kua Nasi’ kuwawezesha wafanyabiashara wadogo – Mwanaharakati Mzalendo
ADVERTISEMENT
  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact
Mwanaharakati Mzalendo
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv
No Result
View All Result
Mwanaharakati Mzalendo
No Result
View All Result
Home BIASHARA

NBC yazindua akaunti ya ‘NBC Kua Nasi’ kuwawezesha wafanyabiashara wadogo

Serikali yaipongeza, yataka iongeze nguvu katika utoaji elimu.

I am Krantz by I am Krantz
Nov 14, 2020
in BIASHARA, HABARI
0 0
0
NBC yazindua akaunti ya ‘NBC Kua Nasi’ kuwawezesha wafanyabiashara wadogo
0
SHARES
76
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter
ADVERTISEMENT

 

 

Mkurugenzi wa Fedha wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) Waziri Barnabas akizungumza wakati wa uzinduzi wa huduma mpya ya benki hiyo ijulikanayo kama ‘NBC Kua Nasi’ ambayo inawawezesha wafanyabiashara wadogo kukuza biashara zao kupitia huduma nafuu za kibenki.Uzinduzi huo ulifanyika katika tawi la benki hiyo Mbagala jijini Dar es Salaam.

 


Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Godwin Gondwe akizungumza na wafanyakazi wa NBC pamoja na wafanyabiashara wadogo wadogo wa Wilaya hiyo wakati benki hiyo ilipozinuda huduma mpya ijulikanayo kama ‘NBC Kua Nasi’.Huduma hiyo inawawezesha wajasiriamali kuweka akiba ya pesa za mauzo kwa unafuu na usalama zaidi.




.


Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Godwin Gondwe na Mkurugenzi wa Fedha wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC), Waziri Barnabas wakizindua huduma mpya ijulikanayo kama ‘NBC Kua Nasi’ katika hafla iliyofanyika kwenye tawi la benki hiyo Mbagala jijini Dar es Salaam.Kushoto ni Abel Kaseko, Mkuu wa Bidhaa na Mauzo wa NBC.AKaunti hiyo ni maalumu kwa wafanyabiashara wadogo kuwawezesha kuweka akiba kwa urahisi zaidi.

Dar es Salaam.Katika kuhakikisha wafanyabiashara wadogo wanakuza biashara zao, benki ya Taifa ya biashara (NBC) imezindua huduma mpya ijulikanayo kama ‘NBC Kua Nasi’ huku Serikali ikiitaka kuongeza juhudi katika utoaji wa elimu ya fedha.


Akaunti ya ‘NBC Kua Nasi inawawezesha wajasiriamali wadogo kutunza pesa zao kwa usalama zaidi bila gharama za uendeshaji.Pia, inaambatana na utoajia wa  elimu ya fedha ili kuwaongezea ufanisi wa uendeshaji wa biashara.


Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Godwin Gondwe alisema hatua hiyo ni muhimu katika utekelezaji wa mipango ya Serikali ikiwamo kuhakikisha kila mtanzania anafikiwa na huduma nafuu za kibenki.


“Akaunti hii ni fursa kwa vijana, akina mama na wajasiriamali wote; kwanza unaweka fedha zako na hakuna malipo ya mwezi.Pili, akaunti hii inaambatana na kutoa elimu ya kibenki, hii ni sehemu ambayo tulikuwa hatujaitilia mkazo hasa kwa wajasiriamali waodogo,” alisema Gondwe.


Aliitaka benki hiyo kuongeza nguvu zaidi katika kuwaelimisha wajasiriamali kufahamu namna bora ya usimamizi wa fedha ili waweze kukua zaidi.


“Mwaka jana tumetoa zaidi ya Sh2.6 bilioni za mikopo kwa wajasiriamali wadogo, hii huduma imekuja wakati muafaka ili waweze kufahamu namna bora zaidi ya kutunza fedha,” alisema.


Mkurugenzi wa Fedha wa NBC, Waziri Barnabas alisema akaunti hiyo inawawezesha wafanyabishara wadogo kukuza biashara zao kwa kuweka pesa kwa urahisi na unafuu kwani huduma hiyo inapatikana mahali popote kwa njia ya simu (NBC Kiganjani).


Alisema kupitia ‘NBC Kua Nasi’ wafanyabiashara wadogo kama mamalishe, madereva bodaboda,wasindikaji pamoja na wasusi wataweza kuhifadhi pesa zao kwa urahisi zaidi na kuacha kukaa na pesa taslimu njia ambayo si salama.


“Makundi haya yanaajiri watu wengi sana na ufikaji wa huduma za kifedha kwao umekuwa mgumu na mara nyingi wanakaa na fedha mkononi hivyo akaunti hii ni sehemu ya mpango wa benki yetu katika kuhakikisha tunawafikia watu wengi zaidi  kuwapatia huduma za kifedha zinazoendana na shughuli zao za kiuchumi,” alisema Barnabas.


Aidha, mteja ataweza kupata riba ya hadi asilimia 2 atakapoweka fedha kwenye akaunti hiyo ndani ya mwaka.


Mmoja wa wafanyabiashara, Dativa Ngowi alisema huduma hiyo itakuwa msaada mkubwa kwa kupunguza gharama za uendeshaji za kila mwezi pamoja na makato ya kutoa pesa.



Tags: NBC
ADVERTISEMENT
I am Krantz

I am Krantz

Related Posts

Walimu wamtoa mimba mwanafunzi, wakamatwa na Polisi
HABARI

Walimu wamtoa mimba mwanafunzi, wakamatwa na Polisi

by Mhariri
Jan 22, 2021
0

Na Amiri Kilagalila,Njombe Jeshi la Polisi mkoani...

Read more
Serikali yajipanga kumaliza changamoto ya uhaba wa mafuta ya kula nchini

Serikali yajipanga kumaliza changamoto ya uhaba wa mafuta ya kula nchini

Jan 22, 2021
Amuua mdogo wake kisa kuku kuingia kwenye shamba lake

Amuua mdogo wake kisa kuku kuingia kwenye shamba lake

Jan 22, 2021
Mkuu wa Majeshi ya Malawi kushiriki mashindano ya Golf ya Johnnie Walker Waitara Trophy

Mkuu wa Majeshi ya Malawi kushiriki mashindano ya Golf ya Johnnie Walker Waitara Trophy

Jan 22, 2021
IGP Sirro akemea vitendo vya udhalilishaji Zanzibar

IGP Sirro akemea vitendo vya udhalilishaji Zanzibar

Jan 22, 2021
Kiwanda cha Twiga Cement wamkabidhi RC Kunenge mifuko 800 ya Saruji

Kiwanda cha Twiga Cement wamkabidhi RC Kunenge mifuko 800 ya Saruji

Jan 22, 2021
Next Post
MIAKA MITANO YA MAAJABU/SITA KUBWA ZA MAGUFULI/USAJILI MPYA SIMBA UTATA

MIAKA MITANO YA MAAJABU/SITA KUBWA ZA MAGUFULI/USAJILI MPYA SIMBA UTATA

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

I agree to the Terms & Conditions and Privacy Policy.

Currently Playing

KRANTZ MWANTEPELE (FOUNDER & CEO)

ADVERTISEMENT

KONCEPT TV

https://www.youtube.com/watch?v=0HP0mB_rtIU&t=7s
ADVERTISEMENT
Mwanaharakati Mzalendo

Mwanaharakati Mzalendo ni mtandao namba moja kwa habari makini kutoka pande zote za dunia kuhusiana na Michezo, Siasa, Afya, Elimu, Mahusiano, Vituko, n.k

Wasiliana nasi kwa Email;krantzcharles@gmail.com
SIMU; 0658123310

Follow Us

November 2020
M T W T F S S
« Oct   Dec »
 1
2345678
9101112131415
16171819202122
23242526272829
30  
Currently Playing
  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

All rights reserved © 2020 Mwanaharakati Mzalendo - Powered by Koncept.

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv

All rights reserved © 2020 Mwanaharakati Mzalendo - Powered by Koncept.

Login to your account below

Forgotten Password?

Fill the forms bellow to register

*By registering into our website, you agree to the Terms & Conditions and Privacy Policy.
All fields are required. Log In

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In