Rais Donald Trump wa Marekani amesemaataondoka Ikulu kama bodi ya wajumbe wa uchaguzi itampigia kura Rais mteule Joe Biden mwezi wa Desemba.
Rasi Trump amesema hayo kwa wanahabari baada ya kufanya mkutano na jeshi la Marekani kusherehekea siku ya Shukrani Thanksgiving kupitia njia ya simu.
Amesema kama bodi hiyo itathibitisha ushindi wa Biden wakati ikifanya mkutano Desemba 14, hakika ataachia madaraka. Ameongeza kuwa itakuwa jambo gumu kutambua hali hiyo. Kama wajumbe hao wakimpigia kura Biden, watafanya kosa kubwa.
Vyombo vya habari vya Marekani vimekadiria kuwa Biden amepata kura 306 za wajumbe wa bodi hiyo, ambazo zimezidi kiwango cha kura 270 cha kushinda uchaguzi.