Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Aboubakar Kunenge ameviagiza vituo vya uuzaji wa Mafuta kuhakikisha wanazingatia leseni za biashara hiyo ikiwa ni pamoja na ubora wa Mafuta, tahadhari za kiusalama kwenye vituo, ubora wa huduma na kuepuka kupandisha gharama za Mafuta kinyume na utaratibu.
RC Kunenge ametoa maelekezo hayo wakati wa uzinduzi wa wiki ya huduma kwa wateja wa vituo vya Mafuta vya Puma Energy ambapo ametoa wito kwa wafanyakazi wanaotoa huduma kuwa na mahusiano mazuri na wateja.
Aidha RC Kunenge amesema sekta ya Mafuta ni muhimu Sana Katika kurahisisha shughuli za kijamii na uchumi hivyo amewahimiza kuzingatia huduma Bora.