Inaripotiwa kuwa kifurushi cha kustaajabisha kilichojaa rubles milioni 50, ambazo ni sawa na dola za kimarekani 673,000 (Tsh. Bilioni 1.56) kilichimbuliwa kutoka kwenye kaburi moja nchini Russia hivi karibuni.
Polisi wamesema kiasi hicho kikubwa cha pesa kilifichwa na mtendaji wa kampuni ya umeme wa eneo hilo ambaye alituhumiwa kupokea rushwa, na tayari mhusika huyo amekamatwa.