Chanjo ya virus vya Corona inayotengenezwa na kampuni ya Astrazeneca na chuo kikuu cha Oxford imepata mafanikio makubwa katika hatua ya Majaribio na sasa iko tayari kuanza kutumika.
Kupitia gazeti la Sunday Times mkuu wa kampuni ya Astrazeneca amethibitisha kuwa chanjo hiyo inaweza kutoa kinga Kwa asilimia 100 dhidi ya virus vya Corona baada ya Majaribio kadhaa.
Chanjo hiyo inaelezwa kufanyiwa tathimini na taasisi ya udhibiti wa dawa nchini Uingereza.
Kwa mujibu wa gazeti hilo chanjo hiyo inaweza kupewa ithibati Leo disemba 28,na tayari Serikali nchini Uingereza imeagiza Dozi million 100 zigawiwe Kwa watu nchini humo.