Hakikisheni bidhaa bandia haziingi nchini – Waziri Mkuu – Mwanaharakati Mzalendo
ADVERTISEMENT
  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact
Mwanaharakati Mzalendo
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv
No Result
View All Result
Mwanaharakati Mzalendo
No Result
View All Result
Home HABARI

Hakikisheni bidhaa bandia haziingi nchini – Waziri Mkuu

Mhariri by Mhariri
Dec 5, 2020
in HABARI
0 0
0
Hakikisheni bidhaa bandia haziingi nchini – Waziri Mkuu
0
SHARES
32
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ameziagiza mamlaka zote za udhibiti zihakikishe kuwa bidhaa zinazoingizwa nchini kwa ajili maonesho mbalimbali zinakuwa na viwango vya kimataifa na pia bidhaa zisizo na viwango na bidhaa bandia hazipati nafasi ya kuingia kwenye soko la Tanzania.

Hata hivyo, Waziri Mkuu amewataka wamiliki wa viwanda wazalishe bidhaa kwa wingi na kwa kutumia malighafi zinazopatikana katika mbalimbali nchini jambo ambalo litawezesha kuwa na uzalishaji wenye gharama ndogo na kuwa na bei shindani katika soko.

Waziri Mkuu ametoa maagizo hayo jana (Ijumaa, Desemba 4, 2020) baada ya kufungua Maonesho ya Tano ya Bidhaa za Viwanda vya Tanzania katika Uwanja wa Maonesho ya Biashara ya Kimataifa wa Mwalimu J. K. Nyerere, Dar-Es-Salaam. Kaulimbiu ya maeneo hayo ni ‘Tumia Bidhaa za Tanzania, Jenga Tanzania.’

“Watanzania tuachane na fikra potofu kuwa bidhaa zinazotoka nje ya nchi ndizo zenye ubora kuliko za hapa nchini, kwani bidhaa zetu ni bora na zina viwango vinavyostahili. Hebu sote tununue bidhaa zetu ili kukuza ajira na pato la mtu binafsi na Taifa kwa ujumla. Sisi Watanzania tunazalisha vitu bora na vyenye uhalisia.”

ADVERTISEMENT

Amesema uwekezaji unaofanywa lazima uzingatie uendelevu, ubora na tija kulingana na viwango vinavyokubalika Kitaifa na Kimataifa katika shughuli za uzalishaji ili kuhimili ushindani na hata kuweza kunufaika na fursa za masoko zinazoendelea kujitokeza. “Nina hakika tukijipanga tutaweza kuwa washindani mahiri na bidhaa zenu zitaingia na kuleta ushindani mkubwa kwenye soko.”

Pia, Waziri Mkuu amewataka wawekezaji na wazalishaji wote nchini wafanye biashara halali, walipe kodi kikamilifu na wahakikishe wanatunza kumbukumbu vizuri ili Serikali iweze kupata takwimu sahihi za biashara zinazofanyika ikiwemo na nchi jirani na kuweza kuandaa sera mahususi za kuwasaidia.

“Wizara ya Viwanda na Biashara hakikisheni wazalishaji wanatumia vizuri sheria za uasilia wa bidhaa ili kuweza kukidhi matakwa na kutumia fursa ya masoko ambayo Serikali yetu imesaini mikataba ya maridhiano hususani soko la Afrika Mashariki, SADC, AGOA na fursa nyingine za masoko ya pamoja.”

Kadhalika, Waziri Mkuu ametumia fursa hiyo kuziagiza Halmashauri zote nchini zihakikishe viwanda vilivyo katika mamlaka zao vinashiriki kuonesha bidhaa wanazozalisha ili bidhaa hizo ziweze kutafutiwa masoko katika nchi mbalimbali duniani zikwemo nchi za Ukanda wa EAC na SADC kwa lengo la kuongeza mauzo ya Tanzania nje ya nchi.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akipewa maelezo na Kijana Mbunifu kutoka SIDO, Joseph Taifa, kuhusu gari kwa ajili ya walemavu wa miguu lililotengenezwa na Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo (SIDO) katika maonesho ya Tano ya Bidhaa za Viwanda vya Tanzania, Leo Disemba 4, 2020 jijini Dar es Salaam.

Pia, Waziri Mkuu ameiagiza Wizara za Fedha na Mipango na Viwanda na Biashara ziendelee na mikakati ya kisera na kikodi ya namna ya kupunguza uagizaji wa baadhi ya bidhaa zinazozalishwa nje na kuongeza ununuzi wa bidhaa zinazozalishwa ndani ili kukuza viwanda vya ndani mfano; bidhaa za mbao, mafuta ya kula na saruji.

“SIDO kwa kushirikiana na VETA wekeni kipaumbele cha kutoa mafunzo na kubuni nyenzo zinazoendana na mahitaji makubwa yaliyomo katika jamii ikiwemo katika eneo la kuchakata mazao kama korosho, chikichi, ufuta, alizeti na matumizi ya TEHAMA katika kuboresha uzalishaji mali, ufanisi, viwango na kutafuta masoko.”

Pia, Waziri Mkuu ameiagiza Wizara ya Viwanda na Biashara pamoja na Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE) kufanya maboresho katika uratibu wa maonesho mbalimbali ya Viwanda na Biashara ili yafanyike kwa kuzingatia kanda za uzalishaji nchini badala ya nguvu kubwa kuelekezwa Dar Es Salaam na miji mikubwa.

ADVERTISEMENT
Mhariri

Mhariri

Related Posts

Rais Magufuli ashuhudia utiaji saini mkataba wa uchimbaji wa madini ya Nickel
HABARI

Rais Magufuli ashuhudia utiaji saini mkataba wa uchimbaji wa madini ya Nickel

by Ombeni Osward
Jan 19, 2021
0

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania...

Read more
Kijana amuua babu yake kumnusuru na mateso

Kijana amuua babu yake kumnusuru na mateso

Jan 19, 2021
Rwanda yaendeleza Lockdown kupunguza maambukizi ya Corona

Rwanda yaendeleza Lockdown kupunguza maambukizi ya Corona

Jan 19, 2021
Lacazette ananisaidia kuongeza ujasiri – Smith Rowe

Lacazette ananisaidia kuongeza ujasiri – Smith Rowe

Jan 19, 2021
Hospitali ya Uhuru yatibu wagonjwa 300

Hospitali ya Uhuru yatibu wagonjwa 300

Jan 19, 2021
Watumishi wa NCAA watakiwa kuweka Malengo ya Utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi ya chama tawala 2020 – 2025

Watumishi wa NCAA watakiwa kuweka Malengo ya Utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi ya chama tawala 2020 – 2025

Jan 19, 2021
Next Post
Bilioni 1.5 yachimbuliwa kutoka kwenye kaburi

Bilioni 1.5 yachimbuliwa kutoka kwenye kaburi

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

I agree to the Terms & Conditions and Privacy Policy.

Currently Playing

KRANTZ MWANTEPELE (FOUNDER & CEO)

ADVERTISEMENT

KONCEPT TV

https://www.youtube.com/watch?v=0HP0mB_rtIU&t=7s
ADVERTISEMENT
Mwanaharakati Mzalendo

Mwanaharakati Mzalendo ni mtandao namba moja kwa habari makini kutoka pande zote za dunia kuhusiana na Michezo, Siasa, Afya, Elimu, Mahusiano, Vituko, n.k

Wasiliana nasi kwa Email;krantzcharles@gmail.com
SIMU; 0658123310

Follow Us

December 2020
M T W T F S S
« Nov   Jan »
 123456
78910111213
14151617181920
21222324252627
28293031  
Currently Playing
  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

All rights reserved © 2020 Mwanaharakati Mzalendo - Powered by Koncept.

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv

All rights reserved © 2020 Mwanaharakati Mzalendo - Powered by Koncept.

Login to your account below

Forgotten Password?

Fill the forms bellow to register

*By registering into our website, you agree to the Terms & Conditions and Privacy Policy.
All fields are required. Log In

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In