IGP Sirro afanya mabadiliko ndani ya Jeshi la Polisi – Mwanaharakati Mzalendo
ADVERTISEMENT
  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact
Mwanaharakati Mzalendo
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv
No Result
View All Result
Mwanaharakati Mzalendo
No Result
View All Result
Home HABARI

IGP Sirro afanya mabadiliko ndani ya Jeshi la Polisi

Mhariri by Mhariri
Dec 4, 2020
in HABARI
0 0
0
IGP Sirro afanya mabadiliko ndani ya Jeshi la Polisi
0
SHARES
42
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini Tanzania, IGP Simon Sirro amefanya mabadiliko ya makamanda wa mikoa ya kipolisi ya Lindi, Morogoro, Tabora na Mkoa wa Kipolisi Kinondoni jijini Dar es Salaam.

Wakati huo huo, IGP Sirro amewahamisha vituo vya kazi maofisa waandamizi wa jeshi hilo nchini.

Msemaji wa jeshi hilo, David Misime amethibitisha hayo jana Desemba 3, 2020 kupitia taarifa aliyoitoa kwa umma.

Ameeleza kuwa, aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, Edward Bukombe amepelekwa makao makuu ya Polisi Kitengo cha Picha na Video.

Aidha, nafasi yake imechukuliwa na Ramadhan Kingai aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi Mkoa wa Arusha.

Wakati huo huo, Kamishna Msaidizi wa Polisi, Wilbroad Mutafungwa ambaye alikuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro amekuwa Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini na nafasi yake imechukuliwa na Kamishna Msaidizi Mwandamizi, Fortunatus Muslim.

ADVERTISEMENT

Pia aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Lindi, Stanley Kulyamo amepelekwa Shule ya Lolisi Moshi mkoani Kilimanjaro kuwa Afisa Mnadhimu wa chuo hicho na nafasi yake ikichukuliwa na Mtatiro Kitinkwi ambaye awali alikuwa Afisa Mnadhimu shuleni hapo.

Pia Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, Barnabas Mwakalukwa amerudishwa makao makuu ya Polisi Dodoma kuwa afisa mnadhimu katika Kamisheni ya Ushirikishwaji wa Jamii na nafasi yake imechukuliwa na Kamishna Msaidizi wa Polisi, Safia Shomari ambaye alikuwa Ofisa Mnadhimu namba moja Mkoa wa Mwanza.

Hata hivyo, katika mabadiliko hayo, IGP Sirro amemhamisha Naibu Kamishna wa Polisi, Mpinga Gyumi kutoka Kitengo cha Ufuatiliaji na Tathmini makao makuu ya polisi Zanzibar na kuwa mkuu wa utawala wa rasilimali watu huku aliyekuwa mkuu wa utawala na rasilimali watu, Faustine Shilogile akipelekwa kuwa naibu mkurugenzi wa upelelezi wa makosa ya jinai makao makuu ya polisi Dodoma.

Kamanda Shilogile amechukua nafasi ya naibu kamishna wa polisi, Charles Kenyella ambaye amestaafu.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Naibu kamishna wa polisi, Lucas Mkondya amehamishwa kutoka idara ya maendeleo ya milki makao makuu ya polisi kuwa kaimu kamishna wa fedha na lojistiki na nafasi yake kuchukuliwa na naibu kamisha wa jeshi hilo, John Gudaba.

ADVERTISEMENT
Mhariri

Mhariri

Related Posts

Dkt.JPM ampongeza Mseveni kushinda Urais
HABARI

Dkt.JPM ampongeza Mseveni kushinda Urais

by Ombeni Osward
Jan 16, 2021
0

Rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania...

Read more
Raia wa Kenya ashikiliwa na TAKUKURU kwa kujaribu kumhonga apatiwe cheti cha COVID 19

Raia wa Kenya ashikiliwa na TAKUKURU kwa kujaribu kumhonga apatiwe cheti cha COVID 19

Jan 16, 2021
Nyumba 6 zaezuliwa na upepo mkali ulioambata na mvua mkoani Njombe

Nyumba 6 zaezuliwa na upepo mkali ulioambata na mvua mkoani Njombe

Jan 16, 2021
Mseveni ashinda Urais tena

Mseveni ashinda Urais tena

Jan 16, 2021
Bilioni 11 zaokolewa chakula cha Wafungwa

Bilioni 11 zaokolewa chakula cha Wafungwa

Jan 16, 2021
Waziri Ndugulile awataka wakuu wa Taasisi zilizochini yake kuwa wabunifu ili kuleta mafanikio

Waziri Ndugulile awataka wakuu wa Taasisi zilizochini yake kuwa wabunifu ili kuleta mafanikio

Jan 16, 2021
Next Post
Unywaji wa maziwa upo kiwango cha chini Tanzania, mtu mmoja atakiwa kunywa lita 200 kwa mwaka

Unywaji wa maziwa upo kiwango cha chini Tanzania, mtu mmoja atakiwa kunywa lita 200 kwa mwaka

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

I agree to the Terms & Conditions and Privacy Policy.

Currently Playing

KRANTZ MWANTEPELE (FOUNDER & CEO)

ADVERTISEMENT

KONCEPT TV

https://www.youtube.com/watch?v=0HP0mB_rtIU&t=7s
ADVERTISEMENT
Mwanaharakati Mzalendo

Mwanaharakati Mzalendo ni mtandao namba moja kwa habari makini kutoka pande zote za dunia kuhusiana na Michezo, Siasa, Afya, Elimu, Mahusiano, Vituko, n.k

Wasiliana nasi kwa Email;krantzcharles@gmail.com
SIMU; 0658123310

Follow Us

December 2020
M T W T F S S
« Nov   Jan »
 123456
78910111213
14151617181920
21222324252627
28293031  
Currently Playing
  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

All rights reserved © 2020 Mwanaharakati Mzalendo - Powered by Koncept.

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv

All rights reserved © 2020 Mwanaharakati Mzalendo - Powered by Koncept.

Login to your account below

Forgotten Password?

Fill the forms bellow to register

*By registering into our website, you agree to the Terms & Conditions and Privacy Policy.
All fields are required. Log In

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In