Nyota wa Liverpool, Diogo Jota amebaini kuwa Cristiano Ronaldo ndie mchezaji aliemvutia tangu utotoni.
Nyota huyo mwenye umri wa miaka 24 ikiwa ni miaka 12 nyuma ya nyota wa Juventus Ronaldo aliiambia The Athletic:
“Nakumbuka Euro 2004 wakati Ureno ilipofika fainali na kwa bahati mbaya tulipoteza. Nilikuwa na miaka saba na naikumbuka vizuri, Cristiano Ronaldo alikuwa shujaa wangu. Wakati huo, alikuwa na miaka 19 lakini alikuwa tayari anacheza kwenye Euro na ubora mzuri sana.
“Wakati wa utoto wangu, alikuwa Manchester United na Real Madrid. Kama vijana wa Ureno, siku zote tulimtazama kama kumbukumbu yetu kuu.”
Hivi sasa wawili hao wanacheza pamoja katika timu ya taifa ya Ureno.