kocha wa zamani wa Tottenham Hotspur Mauricio Pochettino anadhaniwa zaidi kurithi mikoba ya Zinedine Zidane kama Kocha wa Real Madrid, Baada ya kichapo kingine cha aibu cha 2-0 dhidi ya Shakhtar Donetsk Jumanne usiku kwenye usiku wa ligi ya mabingwa ulaya UEFA.
kocha huyo mwenye umri wa miaka 48 alifufutwa kazi na Tottenham Hotspur mnamo Novemba 2019, na amekuwa akihusishwa na kazi kubwa zaidi katika mpira wa miguu tangu wakati huo.
Hisa ya Muargentina huyo bado iko juu licha ya kufukuzwa kazi, baada ya kushindwa katika fainali ya ligi kuu ya mabingwa ulaya (UEFA).
Kituo cha Uhispania (El Mundo) kinaripoti kwamba kocha huyo wa zamani wa Spurs ndiye anadhaniwa kurithi mikoba kutoka kwa Zidane huko Madrid.
Mtu mwingine ambaye anasemekana kuwania mikoba ya zidan Bernabéu ni gwiji wa zamani wa Madrid Raul.
Mshambuliaji huyo wa zamani kwa sasa anasimamia upande wa vijana wa kilabu ya Castilla, na anaweza kupandishwa ili kuokoa jahazi la magwiji hao endapo Zidane ataachia mikoba hiyo.
Real sasa wanashika nafasi ya tatu katika kundi lao, nyuma ya Borussia Monchengladbach na Shakhtar, wakiwa hatarini kuingia katika mashindano ya ligi ya Uropa.
Soka la Ligi ya Uropa sio chaguo kwa Florentino Perez, ambaye inasemekana anaamini historia ya kilabu hiyo itachafuliwa kwa kushiriki mashindano ya sekondari