Jeshi la Polisi Mkoa wa Songwe linamshikilia mwalimu wa shule ya sekondari ya Vwawa wilayani Mbozi, Paschal Vahaye(35) kwa tuhuma za kukutwa na mwafunzi wa kike wa bweni nyumbani kwake nyakati za usiku kwa nia ya kutaka kufanya mapenzi.
Mwalimu huyo alikamatwa akiwa na mwanafunzi huyo wa kidato cha sita (jina limehifadhiwa) baada ya uongozi wa shule hiyo kuweka mtego kutokana na tuhuma za kuwapo kwa baadhi ya walimu katika shule kujihusisha kimapenzi na wanafunzi wao.
Mwanafunzi huyo alikutwa chumbani akiwa mtupu.
Kamanda wa jeshi la Polisi Mkoa wa Songwe, George Kyando, alithibitisha kushikiliwa kwa mwalimu huyo na kusema kuwa tayari jeshi hilo limefungua jalada la uchunguzi.