Raisi mteule wa Marekani Joe Biden ameahidi kuwa akiapishwa atahakikisha wanaanchi nchini humo humo wanavaa barakoa Kwa siku 100 ili kupunguza maambukizi ya virus vya Corona.
Akifanya mahojiano na kituo cha habari CNN alisema kuwa akiapishwa atatoa amri kuhakikisha wananchi wote nchini humo wanavaa barakoa hususa ni katika ofisi za serikali.
“Siku ya Kwanza nikiapishwa nitawaomba wananchi wote kuvaa barakoa Kwa siku 100 tu na sio milele, nadhani hii itasaidia kupunguza Kasi ya maambukizi ya virusi vya corona” Alisema Biden.
Mpaka sasa Marekani inaripotiwa kuwa na zaidi ya visa milioni 2 na watu zaidi ya laki 2 kupoteza maisha kutokana na Corona.