Nyota wa juventus Ronaldo amewashukuru Mashabiki na wachezaji wenzake kumfanya afikishe mabao 750 katika maisha yake ya soka.
Ronaldo alifunga goli hilo dakika ya 57 katika mchezo uliomalizika Kwa Juventus kupata ushindi wa 3-0 dhidi ya Dynamo Kiev kwenye Ligi ya mabingwa barani Ulaya katika kundi G
Kupitia mtandao wa Twitter Ronaldo aliandika.
“Nawashukuru wachezaji, Makocha mlionifanya kufikia hatua hii asante Kwa wote mlionisaidia katika juhudi zangu”.
ushindi wa Juventus umewaweka katika nafasi ya pili kwenye kundi G wakiwa na jumla ya alama 12 ikiwa ni alama 3 nyuma dhidi ya Barcelona walioko kileleni wakiwa na jumla ya alama 15.