Nyota wa kilabu ya Juventus na timu ya taifa ya Ureno Cristiano Ronaldo ametwaa tuzo ya Mchezaji bora wa Karne ya 21 (2001-2020) zilizotelewa na Globe soccer awards usiku wa Disemba 27,2020 huko Dubai.
Ronaldo amewashinda Nyota Leonel Messi, Ronaldinho na Mohammed Salah, aliokuwa akichuana nao kwenye kipengere hicho.
“Ni furaha kushinda mataji,” alisema Ronaldo, katika hafla hiyo.
“Sio rahisi kuwa juu ya mchezo kwa miaka mingi. Ninajivunia sana, lakini bila timu, makocha wakubwa na vilabu isingewezekana.”