TANESCO yapongezwa kwa kuwezesha viwanda nchini – Mwanaharakati Mzalendo
ADVERTISEMENT
  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact
Mwanaharakati Mzalendo
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv
No Result
View All Result
Mwanaharakati Mzalendo
No Result
View All Result
Home HABARI

TANESCO yapongezwa kwa kuwezesha viwanda nchini

Mhariri by Mhariri
Dec 5, 2020
in HABARI
0 0
0
TANESCO yapongezwa kwa kuwezesha viwanda nchini
0
SHARES
39
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa akiwa katika ufunguzi wa Maonesho ya tano ya bidhaa za viwanda vya Tanzania, amelipongeza Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kwa kuwezesha Viwanda vya Tanzania kujiendesha kwa gharama nafuu na kwa umeme wa uhakika.

Waziri Mkuu ameeleza hayo alipotembelea banda la Maonesho la TANESCO lililopo katika Maonesho hayo ya bidhaa za viwanda vya Tanzania yanayofanyika mara moja kwa mwaka ambapo kwa mwaka huu yameanza Tarehe 3 mpaka 9 Disemba.

“TANESCO mnafanya kazi nzuri kuhakikisha viwanda kote nchini vinapata umeme wakutosha, wa uhakika na wa bei nafuu ili wasiwe na kisingizio chochote cha kupandisha bei ya bidhaa zao bila sababu za msingi” amesema Mhe. Majaliwa.

ADVERTISEMENT

Akiwa katika banda la TANESCO, Waziri Mkuu alijionea shughuli na huduma mbalimbali zitolewazo na TANESCO Nchini kote katika kuimarisha na kuendeleza Sekta ndogo ya huduma ya Nishati ya umeme Nchini.

Aidha kwa upande wa wataalamu wa TANESCO waliokuwa katika Maonesho hayo walieleza kuwa kiwango cha uzalishaji Umeme kinakidhi mahitaji yote mpaka na mahitaji ya ziada ambayo yatajitokeza.

“Mpaka sasa umeme unaozalishwa ni mwingi ukilinganisha na matumizi ya juu ya Nchi, hivyo kulifanya Shirika kuwa na uwezo mkubwa wa kuvipatia umeme viwanda vyote na kubakiwa na ziada ya umeme” alisema Mhandisi Edetrude Zenda ambaye ni Afisa Uwekezaji TANESCO.

Katika maonesho hayo TANESCO inatoa elimu kuhusu masuala mbalimbali ya huduma na utekelezwaji wa miradi mikubwa ya kimkakati ukiwemo mradi wa Julius Nyerere MW 2115.

ADVERTISEMENT
Mhariri

Mhariri

Related Posts

Walimu wamtoa mimba mwanafunzi, wakamatwa na Polisi
HABARI

Walimu wamtoa mimba mwanafunzi, wakamatwa na Polisi

by Mhariri
Jan 22, 2021
0

Na Amiri Kilagalila,Njombe Jeshi la Polisi mkoani...

Read more
Serikali yajipanga kumaliza changamoto ya uhaba wa mafuta ya kula nchini

Serikali yajipanga kumaliza changamoto ya uhaba wa mafuta ya kula nchini

Jan 22, 2021
Amuua mdogo wake kisa kuku kuingia kwenye shamba lake

Amuua mdogo wake kisa kuku kuingia kwenye shamba lake

Jan 22, 2021
Mkuu wa Majeshi ya Malawi kushiriki mashindano ya Golf ya Johnnie Walker Waitara Trophy

Mkuu wa Majeshi ya Malawi kushiriki mashindano ya Golf ya Johnnie Walker Waitara Trophy

Jan 22, 2021
IGP Sirro akemea vitendo vya udhalilishaji Zanzibar

IGP Sirro akemea vitendo vya udhalilishaji Zanzibar

Jan 22, 2021
Kiwanda cha Twiga Cement wamkabidhi RC Kunenge mifuko 800 ya Saruji

Kiwanda cha Twiga Cement wamkabidhi RC Kunenge mifuko 800 ya Saruji

Jan 22, 2021
Next Post
Mshindi wa Vodacom Shangwe Shangwena akabidhiwa gari yake mjini Biharamulo

Mshindi wa Vodacom Shangwe Shangwena akabidhiwa gari yake mjini Biharamulo

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

I agree to the Terms & Conditions and Privacy Policy.

Currently Playing

KRANTZ MWANTEPELE (FOUNDER & CEO)

ADVERTISEMENT

KONCEPT TV

https://www.youtube.com/watch?v=0HP0mB_rtIU&t=7s
ADVERTISEMENT
Mwanaharakati Mzalendo

Mwanaharakati Mzalendo ni mtandao namba moja kwa habari makini kutoka pande zote za dunia kuhusiana na Michezo, Siasa, Afya, Elimu, Mahusiano, Vituko, n.k

Wasiliana nasi kwa Email;krantzcharles@gmail.com
SIMU; 0658123310

Follow Us

December 2020
M T W T F S S
« Nov   Jan »
 123456
78910111213
14151617181920
21222324252627
28293031  
Currently Playing
  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

All rights reserved © 2020 Mwanaharakati Mzalendo - Powered by Koncept.

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv

All rights reserved © 2020 Mwanaharakati Mzalendo - Powered by Koncept.

Login to your account below

Forgotten Password?

Fill the forms bellow to register

*By registering into our website, you agree to the Terms & Conditions and Privacy Policy.
All fields are required. Log In

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In