Video: Uhamiaji watoa onyo kali wanaoingiza wahamiaji haramu nchini – Mwanaharakati Mzalendo
ADVERTISEMENT
  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact
Mwanaharakati Mzalendo
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv
No Result
View All Result
Mwanaharakati Mzalendo
No Result
View All Result
Home HABARI

Video: Uhamiaji watoa onyo kali wanaoingiza wahamiaji haramu nchini

Mhariri by Mhariri
Dec 4, 2020
in HABARI
0 0
0
Video: Uhamiaji watoa onyo kali wanaoingiza wahamiaji haramu nchini
0
SHARES
35
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Kamishna Jenerali wa Uhamiaji hapa nchini Dkt Annah Makakala amewaonya wananchi wanaojihusisha na biashara haramu ya usafirishaji wa wabinadamu, wahamiaji haramu kuacha mara moja kwani vitendo hivyo ni hatari kwa usalama wanchi na raia wake.

Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dodoma Kamishna jenerali wa Uhamiaji Dkt Annah Makakala amesema kitendo cha kuingiza raia wa kigeni hapa nchini kinyemela ni jambo la hatari sana kwa usalama wanchi.

“Hivi karibuni kumekuwa na ongezeko la wahamiaji haramu wanaoingia nchini kwa makundi kupitia njia zisizo rasmi wakitoka katika pembe ya Afrika, tumepata taarifa kuwa wahamiaji hao wanasaidiwa na baadhi ya wananchi wasiokuwa wazalendo kwa nchi yao” amesema Dkt Annah Makakala.

Amesema kitendo cha wananchi hao kuendelea na biashara hiyo haramu ni hatari kwa sababu wahamiaji wengi wanapoingia huanza matukio ya kihalifu na kutumia siraha pia wanaikoseshea mapato serikali yao, huku akitaja nchi za Ethiopia, Eritria na Somalia ndizo zinazoongoza.

Amesema jeshi la uhamiaji kwa kushirikiana na vyombo vingine vya usalama wataendelea kufuatilia baadhi ya wananchi ambao wanajihusisha na vitendo hivyo na pindi wakibainika kufanya uhalifu huo watachukuliwa hatua za kisheria ambapo adhabu yake ni kifungo miaka 20 au faini ya shilingi million 20 au vyote kwa pamoja.

ADVERTISEMENT

Ameongeza kuwa kwa kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama tangu mwezi Januari hadi Novemba, 2020 wamefanikiwa kuwa kamata raia 45 wa Tanzania wanaojihusisha na vitendo hivyo pamoja na kushikilia magari 13, Boti 2 na pikipiki 16 zinazojihusisha na biashara hiyo.

Aidha amesema kwa kipindi hicho wamefanikiwa kuwakamata wahamiaji haramu 15, 266 ambao waliingia hapa nchini bila kufuata taratibu za kiuhamiaji na tayari wamechukuliwa hatua mbalimbali za kisheria ikiwamo kufikishwa mahakamani.

Katika kukabiliana na tatizo la uhamiaji harama wanatarajia kuanza kutoa elimu katika shule ngazi zote ili kukomesha tatizo hilo watoto wanapokua wajue madhara ya kuingiza wahamiaji haramu ni kosa pia ni hatari kwa usalama wa nchi.

ADVERTISEMENT
Mhariri

Mhariri

Related Posts

Anayedaiwa kumnasa makofi mzazi akutwa na hatia
HABARI

Anayedaiwa kumnasa makofi mzazi akutwa na hatia

by Mhariri
Jan 23, 2021
0

Na WAMJW-Sumbawanga Baraza la Uuguzi na Ukunga...

Read more
TANZIA: Brigedia Jenerali Emmanuel Edward Maganga (Mstaafu) afariki dunia

TANZIA: Brigedia Jenerali Emmanuel Edward Maganga (Mstaafu) afariki dunia

Jan 23, 2021
Magari sita ya wizi yakamatwa Njombe (+video)

Magari sita ya wizi yakamatwa Njombe (+video)

Jan 23, 2021
Walimu wamtoa mimba mwanafunzi, wakamatwa na Polisi

Walimu wamtoa mimba mwanafunzi, wakamatwa na Polisi

Jan 22, 2021
Serikali yajipanga kumaliza changamoto ya uhaba wa mafuta ya kula nchini

Serikali yajipanga kumaliza changamoto ya uhaba wa mafuta ya kula nchini

Jan 22, 2021
Amuua mdogo wake kisa kuku kuingia kwenye shamba lake

Amuua mdogo wake kisa kuku kuingia kwenye shamba lake

Jan 22, 2021
Next Post
Makamu wa Rais akutana na wakandarasi wanawake nchini

Makamu wa Rais akutana na wakandarasi wanawake nchini

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

I agree to the Terms & Conditions and Privacy Policy.

Currently Playing

KRANTZ MWANTEPELE (FOUNDER & CEO)

ADVERTISEMENT

KONCEPT TV

https://www.youtube.com/watch?v=0HP0mB_rtIU&t=7s
ADVERTISEMENT
Mwanaharakati Mzalendo

Mwanaharakati Mzalendo ni mtandao namba moja kwa habari makini kutoka pande zote za dunia kuhusiana na Michezo, Siasa, Afya, Elimu, Mahusiano, Vituko, n.k

Wasiliana nasi kwa Email;krantzcharles@gmail.com
SIMU; 0658123310

Follow Us

December 2020
M T W T F S S
« Nov   Jan »
 123456
78910111213
14151617181920
21222324252627
28293031  
Currently Playing
  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

All rights reserved © 2020 Mwanaharakati Mzalendo - Powered by Koncept.

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv

All rights reserved © 2020 Mwanaharakati Mzalendo - Powered by Koncept.

Login to your account below

Forgotten Password?

Fill the forms bellow to register

*By registering into our website, you agree to the Terms & Conditions and Privacy Policy.
All fields are required. Log In

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In