Unywaji wa maziwa upo kiwango cha chini Tanzania, mtu mmoja atakiwa kunywa lita 200 kwa mwaka – Mwanaharakati Mzalendo
ADVERTISEMENT
  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact
Mwanaharakati Mzalendo
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv
No Result
View All Result
Mwanaharakati Mzalendo
No Result
View All Result
Home HABARI

Unywaji wa maziwa upo kiwango cha chini Tanzania, mtu mmoja atakiwa kunywa lita 200 kwa mwaka

Mhariri by Mhariri
Dec 4, 2020
in HABARI
0 0
0
Unywaji wa maziwa upo kiwango cha chini Tanzania, mtu mmoja atakiwa kunywa lita 200 kwa mwaka
0
SHARES
39
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi anayeshughulikia Mifugo Prof. Elisante Ole Gabriel amesema uzalishaji wa maziwa nchini unazidi kuongezeka kutoka lita bilioni 2.7 kwa mwaka hadi lita bilioni 3.01, huku matumizi ya maziwa yakiripotiwa kuwa bado yako chini.

Akizungumza alipotembelea kiwanda cha Galaxy Food and Beverages Limited kilichopo Mkoani Arusha ili kujionea namna viwanda vya maziwa vinavyozingatia ubora wa bidhaa wanazozalisha, Prof. Gabriel amesema bado jitihada zinatakuwa katika kuhamasisha wananchi kunywa maziwa katika kuboresha afya zao.

“Matumizi ya maziwa nchini ni lita milioni nane kwa siku, ambapo kwa mujibu wa Shirika la Chakula na Kilimo Duniani (FAO) kila mtu anatakiwa kunywa lita 200 kwa mwaka lakini kwa Tanzania unywaji wa maziwa kwa mtu umefikia walau lita 54 kwa mwaka, natoa wito kwa watanzania waongeze bidii katika matumizi ya maziwa kwa ajili ya kuboresha afya zao kwa maana ya akili na uimara wa mwili.” Amesema Prof. Gabriel

Prof. Gabriel ametoa wito kwa sekta binafsi hususan waliopo kwenye tasnia ya maziwa nchini, kuendelea kuiunga mkono serikali kwa kuhakikisha wanaongeza thamani ya bidhaa zao pamoja na kuziweka kwenye vifungashio tofauti kulingana na mahitaji ya wateja wao.

Aidha, amesema Wizara ya Mifugo na Uvuvi inahakikisha inaboresha kosaafu na mbari ya mifugo kwa kutumia njia ya uhimilishaji ili azaliwe ng’ombe mwenye ubora, pia kuzingatia afya ya mifugo kwa kutoa chanjo na mifugo kuogeshwa pamoja na uwepo wa malisho bora.

Pia, ametoa wito kwa wenye viwanda vya maziwa nchini kuhakikisha wanafikia uwezo wa kiwanda uliosimikwa katika uzalishaji wa maziwa kwa kuwa ni hasara kuzalisha kidogo tofauti na uwezo wa kiwanda kwani kwa kufanya hivyo wenye viwanda wanapata hasara na pia serikali inapata mapato kidogo kutokana na tozo mbalimbali.

ADVERTISEMENT

Amewakumbusha pia wenye viwanda vya maziwa kuzalisha bidhaa bora ili watanzania wawe na imani na viwanda vyao na kutumia bidhaa zinazozalishwa hapa nchini kwani kwa kufanya hivyo ajira zitaongezeka pamoja na mapato ya serikali.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Kiwanda cha Galaxy Food and Beverages Limited Bw. Irfhan Virjee amemwambia katibu mkuu huyo kuwa Tanzania inatakiwa iwe nchi ya pili kwa kuzalisha maziwa mengi na kusambaza katika nchi mbalimbali, kwa kuwa ni nchi ya pili barani Afrika kwa kuwa na mifugo mingi na kwamba soko la maziwa bado ni kubwa.

Bw. Virjee ameishukuru serikali kwa kuboresha mazingira ya uwekezaji kwa kuwa kiwanda hicho kimeanzishwa katika serikali ya awamu ya tano na kubainisha kuwa uzalishaji utazidi kuongezeka kutokana na uwepo wa masoko kutoka ndani na nje ya nchi.

ADVERTISEMENT
Mhariri

Mhariri

Related Posts

IGP Sirro akemea vitendo vya udhalilishaji Zanzibar
HABARI

IGP Sirro akemea vitendo vya udhalilishaji Zanzibar

by Mhariri
Jan 22, 2021
0

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP...

Read more
Kiwanda cha Twiga Cement wamkabidhi RC Kunenge mifuko 800 ya Saruji

Kiwanda cha Twiga Cement wamkabidhi RC Kunenge mifuko 800 ya Saruji

Jan 22, 2021
Naibu Waziri Kipanga aagiza Vyuo vya VETA kwenye Wilaya 25 vyote vikamilike kwa wakati

Naibu Waziri Kipanga aagiza Vyuo vya VETA kwenye Wilaya 25 vyote vikamilike kwa wakati

Jan 22, 2021
Wakurugenzi watakiwa kujitathimini Ukusanyaji wa Mapato (+video)

Wakurugenzi watakiwa kujitathimini Ukusanyaji wa Mapato (+video)

Jan 22, 2021
Rais wa Zanzibar akutana na IGP Sirro

Rais wa Zanzibar akutana na IGP Sirro

Jan 22, 2021
Waziri Aweso awaagiza SUMAJKT kuongeza nguvu kazi kwenye ujenzi wa tanki la Maji Chamwino

Waziri Aweso awaagiza SUMAJKT kuongeza nguvu kazi kwenye ujenzi wa tanki la Maji Chamwino

Jan 22, 2021
Next Post
Ukame wapelekea Namibia kuuza Tembo wake 170

Ukame wapelekea Namibia kuuza Tembo wake 170

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

I agree to the Terms & Conditions and Privacy Policy.

Currently Playing

KRANTZ MWANTEPELE (FOUNDER & CEO)

ADVERTISEMENT

KONCEPT TV

https://www.youtube.com/watch?v=0HP0mB_rtIU&t=7s
ADVERTISEMENT
Mwanaharakati Mzalendo

Mwanaharakati Mzalendo ni mtandao namba moja kwa habari makini kutoka pande zote za dunia kuhusiana na Michezo, Siasa, Afya, Elimu, Mahusiano, Vituko, n.k

Wasiliana nasi kwa Email;krantzcharles@gmail.com
SIMU; 0658123310

Follow Us

December 2020
M T W T F S S
« Nov   Jan »
 123456
78910111213
14151617181920
21222324252627
28293031  
Currently Playing
  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

All rights reserved © 2020 Mwanaharakati Mzalendo - Powered by Koncept.

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv

All rights reserved © 2020 Mwanaharakati Mzalendo - Powered by Koncept.

Login to your account below

Forgotten Password?

Fill the forms bellow to register

*By registering into our website, you agree to the Terms & Conditions and Privacy Policy.
All fields are required. Log In

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In