BODI ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) imetangaza orodha ya awamu ya tatu yenye jumla ya wanafunzi wapya 3,544 waliopangiwa mikopo kwa mara ya kwanza katika mwaka wa masomo 2020/2021, yenye thamani ya Sh bilioni 11.04.
Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB, Abdul-Razaq Badru ilisema ili kupata taarifa za kina kuhusu mikopo waliyopangiwa, wanafunzi hao 3,544 wanashauriwa kutembelea akaunti zao walizotumia kuomba mikopo kwa njia ya mtandao maarufu kama Student’s Individual Permanent Account (SIPA).
“Baada ya kutolewa kwa awamu hii ya tatu, hadi sasa jumla ya wanafunzi wa mwaka wa kwanza waliopangiwa mikopo ni 53,364 yenye thamani ya Sh bilioni 173.29,” amesema Badru.