Wananchi wilayani Nyamagana mkoani Mwanza wametoa kero zao wakimuomba Mbunge wa jimbo la Nyamagana Ndg. Stanslaus Mabula aweze kuwakumbuka katika miundimbinu mbalimbali ikiwemo ujenzi wa barabara ili kuweza kufanikisha utendaji wa kazi kirahisi.
Wengi wao wamelalamikia kuhusu ndoa zao kuvunjika kutokana na kushindwa kuwatimizia mahitaji yao, juu ya miundombinu hafifu ikiwemo kuchelewa kurudi majumbani mwao.
Meneja wa TLULA mkoani humo Eng. Mohamed Mhanda akiongea na wananchi jijini humo ameahidi kuwa barabara hizo zipo kwenye mpango wa serikali na tayari washaweka bajeti
“Changamoto nimeziona lakini tushaweka ahadi kuwa barabara hizi tutazitengeneza mwaka huu wa fedha jumla ya bajeti kukamilisha miradi hiyo ni Bilioni 3 milion 442 na tunatarajia kukamilisha miradi hii mwishoni mwa mwezi wa tano”
Aidha Eng.Mhanda ameahidi kushirikiana na viongozi wa serikali ili kukamirisha miradi hiyo kwa wakati na kwa viwango bora.