Watanzania wakaribishwa maonesho ya tano ya bidhaa za viwanda vya Tanzania – Mwanaharakati Mzalendo
ADVERTISEMENT
  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact
Mwanaharakati Mzalendo
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv
No Result
View All Result
Mwanaharakati Mzalendo
No Result
View All Result
Home HABARI

Watanzania wakaribishwa maonesho ya tano ya bidhaa za viwanda vya Tanzania

Mhariri by Mhariri
Dec 2, 2020
in HABARI
0 0
0
Watanzania wakaribishwa maonesho ya tano ya bidhaa za viwanda vya Tanzania
0
SHARES
39
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Wizara ya Viwanda,na Biashara kupitia taasisi yake ya Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) inawakaribisha Watanzania wote kutembelea Maonesho ya Tano ya Bidhaa za Viwanda vya Tanzania yatakayoanza tarehe 3 hadi 9 Desemba, 2020.

Uanzishwaji wa Maonesho haya yalilenga kuhakikisha Ujenzi wa Uchumi wa Viwanda unakuwa na matokeo chanya katika uchumi na yanayoonekana.

Maonesho haya yanalenga kujenga jukwaa kwa Wadau wa Sekta ya Viwanda kupata fursa ya kujadiliana, kubadilishana uzoefu na kutangaza fursa zilizopo katika Sekta hiyo. Aidha,

ADVERTISEMENT

Maonesho hayo hususan, yanalenga kutoa fursa zifuatazo:-

i. Kuvitambua viwanda vya Tanzania pamoja na bidhaa zinazozalishwa nchini ili Watanzania wazitambue na kupenda kuzitumia;

ii. Kuhamasisha Watanzania kutumia bidhaa na huduma zinazozalishwa hapa nchini;
iii. Kuwaunganisha wenye Viwanda na Wazalishaji mbalimbali wa Malighafi na huduma zingine zinazotumika viwandani; na

iv. Kuwaunganisha wenye Viwanda na Wasambazaji wa teknolojia za
viwanda.

Kauli Mbiu ya Maonesho haya ni “Tumia Bidhaa za Tanzania, Jenga Tanzania” ikiwa ni kuhamasisha Watanzania waendelee kupenda, kununua na kutumia bidhaa zinazozalishwa na viwanda vya Tanzania kwa lengo la kuchochea uzalishaji katika sekta mbalimbali za kiuchumi ili kukuza soko la ndani na hatimaye kuiwezesha Tanzania ambayo imeingia katika Uchumi wa Kati.

Pia, Maonesho haya yataenda sambamba na matukio mbali mbali kama ifuatavyo:-

i. Tarehe 5 Desemba, 2020 kutakuwa na Mkutano kati ya Wizara ya Viwanda na Biashara, Wamiliki wa Viwanda nchini na Taasisi za Uthibiti. Mkutano huu utalenga kutatua changamoto zinazowakabili wamiliki wa viwanda katika uendeshaji wa shughuli za uzalishaji wa bidhaa nchini.
ii.
iii. Tarehe 6 Desemba, 2020 kutakuwa na Bonanza la Maziwa litakalo husisha matembezi ya Afya (Jogging) na michezo mbalimbali. Lengo la kuwa na Bonanza la Maziwa ni kuhamasisha unywaji wa maziwa yanayozalishwa na Viwanda vya Tanzania.

Washiriki na Watembeleaji wa Maonesho watapata kuvitambua na kunywa maziwa kutoka viwanda vyetu vya ndani. Zoezi hili linahamasisha matumizi ya bidhaa za maziwa yanayozalishwa nchini.

iv. Tarehe 7 Desemba, 2020 kutakuwa na kongamano la biashara lenye kuelezea fursa za biashara katika nchi za Dubai, Falme za Kiarabu na Kuwait litakaloenda sambamba na mikutano ya biashara ya ana kwa ana (B2B Meeting) na

v. Huduma ya kliniki ya biashara itatolewa kuanzia tarehe 3 hadi 9 Desemba, 2020 ambapo taasisi zinazosimamia mnyororo wa biashara nchini zitasikiliza na kutatua kero/changamoto za wazalishaji wa bidhaa za Tanzania ana kwa ana Mabanda ya yatafunguliwa saa 4 kamili asubuhi hadi saa 12 Jioni, hakuna kiingilio kwa
watembeleaji. Wote mnakaribishwa.

ADVERTISEMENT
Mhariri

Mhariri

Related Posts

NMB yatoa msaada wa mabati kutekeleza agizo la Waziri Mkuu
HABARI

NMB yatoa msaada wa mabati kutekeleza agizo la Waziri Mkuu

by I am Krantz
Jan 15, 2021
0

 Mkuu wa Wilaya ya Urambo, Angelina Nkwingwa...

Read more
RC Mahenge aliagiza Jiji la Dodoma kudhibiti Ujenzi Holela wa makazi

RC Mahenge aliagiza Jiji la Dodoma kudhibiti Ujenzi Holela wa makazi

Jan 15, 2021
Picha: Makamu wa Rais aongoza kikao cha Baraza la Mawaziri Chamwino Dodoma

Picha: Makamu wa Rais aongoza kikao cha Baraza la Mawaziri Chamwino Dodoma

Jan 15, 2021
NECTA yatangaza matokeo ya kidato cha nne, zijue shule 10 zilizoongoza

NECTA yatangaza matokeo ya kidato cha nne, zijue shule 10 zilizoongoza

Jan 15, 2021
Kisa cha kweli: Mapenzi ya Chuo yawachanganya, waenda kanisani kula kiapo

Kisa cha kweli: Mapenzi ya Chuo yawachanganya, waenda kanisani kula kiapo

Jan 15, 2021
Rais wa Uturuki apewa chanjo ya Corona

Rais wa Uturuki apewa chanjo ya Corona

Jan 15, 2021
Next Post
Video: Jamii yatakiwa kutowanyanyapaa watu wenye ulemavu

Video: Jamii yatakiwa kutowanyanyapaa watu wenye ulemavu

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

I agree to the Terms & Conditions and Privacy Policy.

Currently Playing

KRANTZ MWANTEPELE (FOUNDER & CEO)

ADVERTISEMENT

KONCEPT TV

https://www.youtube.com/watch?v=0HP0mB_rtIU&t=7s
ADVERTISEMENT
Mwanaharakati Mzalendo

Mwanaharakati Mzalendo ni mtandao namba moja kwa habari makini kutoka pande zote za dunia kuhusiana na Michezo, Siasa, Afya, Elimu, Mahusiano, Vituko, n.k

Wasiliana nasi kwa Email;krantzcharles@gmail.com
SIMU; 0658123310

Follow Us

December 2020
M T W T F S S
« Nov   Jan »
 123456
78910111213
14151617181920
21222324252627
28293031  
Currently Playing
  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

All rights reserved © 2020 Mwanaharakati Mzalendo - Powered by Koncept.

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv

All rights reserved © 2020 Mwanaharakati Mzalendo - Powered by Koncept.

Login to your account below

Forgotten Password?

Fill the forms bellow to register

*By registering into our website, you agree to the Terms & Conditions and Privacy Policy.
All fields are required. Log In

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In