Waziri Mkuu ashuhudia MV Kilindoni ikiwekwa Majini – Mwanaharakati Mzalendo
ADVERTISEMENT
  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact
Mwanaharakati Mzalendo
ADVERTISEMENT
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv
No Result
View All Result
Mwanaharakati Mzalendo
No Result
View All Result
Home HABARI

Waziri Mkuu ashuhudia MV Kilindoni ikiwekwa Majini

Mhariri by Mhariri
Dec 15, 2020
in HABARI
0 0
0
0
SHARES
112
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali ya awamu ya tano itaendelea kusimamia utekelezaji wa miradi ya maendeleo ili kuhakikisha inatekelezwa kwa viwango na kuwanufaisha watumiaji.

Waziri Mkuu amesema hayo (Jumanne, Desemba 15, 2020) wakati aliposhuhudia uingizwaji majini wa Kivuko cha MV Kilindoni ‘Hapa kazi Tu’ kitakachofanya safari zake kati ya Nyamisati na Mafia, tukio hilo limefanyika Karakana ya Kujenga na Kukarabati vivuko ya Songoro iliyopo Kigamboni, jijini Dar es salaam

Waziri Mkuu amesema kuwa ujenzi wa kivuko hicho unatokana na ustashi wa Rais, Dkt. John Pombe Magufuli kuhakikisha kwamba ahadi zote zilizowekwa kwenye Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) ya Mwaka 2020-2025 ili Watanzania waweze kuthibitisha kuwa CCM inaahidi na kutekeleza.

“Kwenye Ilani ya 2015-2020, Chama cha Mapinduzi kilisema na kuandika kwamba kutakuwa na kivuko cha kwenda Mafia, hii hapa leo inaingia majini tukiishuhudia kuelekea mafia.”

Aidha, Waziri Mkuu alisema kuwa katika kuhakikisha sekta ya majini inaimarishwa, Serikali imepanga kujenga meli itakayokuwa inafanya kazi katika ukanda wa bahari kutoka bandari ya Mtwara kupitia bandari ndogondogo za Lindi, Kilwa kuja Dar es Salaam, Tanga, Zanzibar pamoja na visiwa jirani vya Comoro.

Waziri Mkuu alifafanua kuwa lengo la Serikali ni kuhakikisha inaimarisha sekta za usafirishaji za barabara, anga, majini pamoja ya reli ili kuwawezesha Watanzania kuchagua aina ya usafiri wanaoutaka.

Awali, Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Umeme na Ufundi Serikalini (TEMESA), Mhandisi Japhet Masele alisema kuwa wakala huo katika mwaka wa fedha 2019-2020 ilikuwa inatekeleza ujenzi wa vivuko vinne na mpaka sasa vivuko vitatu vya MV Ilemela, MV Kayenze na MV Ukara vimeanza kutoa huduma huku MV Kilindoni ndio kimeingia majini kwa mara ya kwanza.

Amesema kuwa Kivuko kipya cha MV Chato kimekamilika na kinatarajiwa kuanza kazi baada ya ukaguzi wa mwisho unaoendelea kufanywa sasa na wataalam kutoka DMI na TASAC.

Kwa upande wake, Naibu Waziri Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia na Mbunge wa Mafia, Mhe. Omary Juma Kipanga amesema kuwa anamshukuru Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa kuwaheshimisa Wana-Mafia kwa kuhakikisha wanapata usafiri wa uhakika na salama.

Kivuko hicho cha MV Kilindoni kitakuwa na uwezo wa kubeba tani 100, yaani abiria 200, magari madogo sita.

Mhariri

Mhariri

Related Posts

Millicom International inayozimiliki Tigo na Zantel yatangaza kuziuza  kwa Axian consortium
HABARI

Millicom International inayozimiliki Tigo na Zantel yatangaza kuziuza kwa Axian consortium

by I am Krantz
Apr 19, 2021
0

Millicom International inayozimiliki Tigo na Zantel yatangaza...

Read more

Mwanangu kaacha kutumia pombe na dawa za kulevya, hivi ndivyo alivyosaidika

Apr 19, 2021
Waziri Mwambe ahimiza Watanzania kuunga mkono Benki ya CRDB asema ni Benki ya kizalendo yenye nia ya dhati ya kuwakomboaa wananchi kiuchumi

Waziri Mwambe ahimiza Watanzania kuunga mkono Benki ya CRDB asema ni Benki ya kizalendo yenye nia ya dhati ya kuwakomboaa wananchi kiuchumi

Apr 19, 2021
Waajiri Serikalini Watakiwa Kuwa Na Mabaraza Ya Wafanyakazi Yanayofanya Kazi Kikamilifu

Waajiri Serikalini Watakiwa Kuwa Na Mabaraza Ya Wafanyakazi Yanayofanya Kazi Kikamilifu

Apr 16, 2021
Balozi Mulamula Apokea Nakala Ya Hati Za Utambulisho Kutoka Kwa Balozi Mteule Wa Uturuki

Balozi Mulamula Apokea Nakala Ya Hati Za Utambulisho Kutoka Kwa Balozi Mteule Wa Uturuki

Apr 16, 2021
Mapenzi ya Chuo yawachanganya, waenda kanisani kula kiapo

Mapenzi ya Chuo yawachanganya, waenda kanisani kula kiapo

Apr 16, 2021
Next Post
UTATA KAMPUNI YA QNET/SIMBA YAVAMIA HARARE KIBABE……..MAGAZETINI LEO JUMATANO TAREHE 16

UTATA KAMPUNI YA QNET/SIMBA YAVAMIA HARARE KIBABE........MAGAZETINI LEO JUMATANO TAREHE 16

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

I agree to the Terms & Conditions and Privacy Policy.

Currently Playing

KRANTZ MWANTEPELE (FOUNDER & CEO)

ADVERTISEMENT

KONCEPT TV

https://www.youtube.com/watch?v=0HP0mB_rtIU&t=7s
Mwanaharakati Mzalendo

Mwanaharakati Mzalendo ni mtandao namba moja kwa habari makini kutoka pande zote za dunia kuhusiana na Michezo, Siasa, Afya, Elimu, Mahusiano, Vituko, n.k

Wasiliana nasi kwa Email;krantzcharles@gmail.com
SIMU; 0658123310

Follow Us

December 2020
M T W T F S S
« Nov   Jan »
 123456
78910111213
14151617181920
21222324252627
28293031  
Currently Playing
  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

All rights reserved © 2020 Mwanaharakati Mzalendo - Powered by Koncept.

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv

All rights reserved © 2020 Mwanaharakati Mzalendo - Powered by Koncept.

Login to your account below

Forgotten Password?

Fill the forms bellow to register

*By registering into our website, you agree to the Terms & Conditions and Privacy Policy.
All fields are required. Log In

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In