Mwenyekiti wa Ngome ya vijana ACT Wazalendo Abdul Nondo, amesema kuwa ACT imejipanga katika kutetea wanufaika wa mkopo unaotolewa na bodi ya mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya juu Tanzania HESLB, ili kuweza kupunguzwa kwa ukubwa wa deni hilo.
Akiongea na waandishi wa habari leo katika ofisi za ACT Wazalendo zilizopo kijitonyama, ametolea ufafanuzi wa sheria iliyowekwa na bodi ya mikopo ya mwaka 2016, na kudai kuwa sheria hiyo inakiuka katiba ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ibara ya 23 (1), inayomtaka mtu kulipwa ujira kutokana na kazi unayoifanya.
Ngome ya ACT Wazalendo wamedhamiria kufungua kesi ili kuwepo kwa marekebisho ya sheria hiyo ili kupunguza makato ya fedha hizo. kwa lengo la kupunguza ukubwa deni hilo, na changamoto zinazowakabiri wanufaika hao.
Aidha ameiomba serikali kupunguza asilimia za makato na adhabu zinazotokana na mkopo huo kitendo kinachowafanya watu kukwepa kulipa fedha hizo
Kuweka wazi ufafanuzi wa asilimia zinazokatwa katika ujira wao ili kuwafanya wanufaika wasilikimbie deni hilo.
Wakati huo huo Nondo ameeleza mikakati iliyoandaliwa na chama hicho katika kuwatetea wanufaika wa mikopo hiyo ikiwemo kushirikiana na wadau mbalimbali kwaajili ya kupigania mabadiriko ya deni hilo.
Kukosoa kwa kupereka barua mamlaka husika ili kuzitatua changamoto zinazowakabiri wahanga wa mkopo huo.
Kutumia wabunge walioteuliwa kuhoji juu ya changamoto hizo na kupinga sheria za mkopo.