Anayedaiwa kumnasa makofi mzazi akutwa na hatia – Mwanaharakati Mzalendo
  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact
Mwanaharakati Mzalendo
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv
No Result
View All Result
Mwanaharakati Mzalendo
No Result
View All Result
Home HABARI

Anayedaiwa kumnasa makofi mzazi akutwa na hatia

Mhariri by Mhariri
Jan 23, 2021
in HABARI
0 0
0
Anayedaiwa kumnasa makofi mzazi akutwa na hatia
0
SHARES
28
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na WAMJW-Sumbawanga

Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania limemkuta na hatia Muuguzi Valentine Kinyanga wa kituo cha afya Mazwi ambaye alilalamikiwa kwa kosa la kumpiga vibao mama aliyefika kujifungua kituoni hapo mnamo tarehe 5 Januari, mwaka huu.

Akisoma hukumu hiyo jana mbele ya wakili wa Serikali Fortunatus Mwandu, Mwenyekiti wa Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania Abner Mathube alisema kuwa Baraza limemtia hatiani mlalalamikiwa chini ya kifungu 26(a)(c) ya sheria ya uuguzi na ukunga kwa kosa la kwanza na la pili.

Mathube alisema kuwa baraza lilichambua maelezo ya mlalamikiwa, mlalamikaji pamoja na mashahidi kuhusu kosa la kwanza la kumpiga mgonjwa kinyume na kifungu 25(3)(c)cha sheria ya uuguzi na ukunga Tanzania.

Katika kosa la kwanza lililotolewa ushahidi ulithibitisha kuwa ni kweli mlalamikiwa alimpiga mlalamikaji na mtuhumiwa alikiri kumpiga mlalamikaji

Aidha, kosa la pili lilikuwa ni kushindwa kusimamia maadili na weledi wa kitaaluma kinyume na kifungu 25(3)(k) lilithibitika kwa mtuhumiwa kushindwa kufuata utaratibu wa utoaji wa huduma za uuguzi na ukunga kwa mlalamikaji, kushindwa kuchukua na kuhifadhi taarifa za vipimo vya mgonjwa, kushindwa kufuatilia mwenendo wa uchungu wa mgonjwa wakati wa kumpokea katika kituo cha kutolea huduma na kuruhusu mtu ambaye sio mtaaluma kumpima mlalamikaji(mgonjwa).

“Kwa kuzingatia utetezi wa mlalamikiwa na ushahidi uliotolewa na mlalamikaji na mashahidi, umethibitisha mashitaka yote kama alivyo shatakiwa na mlalamikaji na kwa kuangalia uzito wa makosa yaliyobainishwa dhidi ya mlalamikaji ya kwamba angeweza kusababisha madhara makubwa kwa kumchapa vibao mama ambaye alikua tayari amejifungua pasipo msaada wake,Muuguzi huyo alipaswa kumuhudumia kwa kwa weledi na upendo mkubwa”.

Aliongeza kuwa kutokana na hayo Baraza limempa adhabu ya kumuondoa kwenye orodha (Rolls) ya wauguzi na wakunga Tanzania chini ya kifungu 28(3)(a) cha sheria ya uuguzi na ukunga Tanzania ya mwaka 2010 na kutakiwa kurejesha vyeti na leseni kwa muuguzi mkuu wa mkoa wa Rukwa ambaye atawasilisha kwa Baraza.

Hata hivyo Mwenyekiti huyo alisema haki ya rufaa imeelezwa…

Mhariri

Mhariri

Related Posts

SIMULIZI; Nilivyolinda Familia Yangu Isikamatwe Wakati Wakitengeneza Pombe
HABARI

SIMULIZI; Nilivyolinda Familia Yangu Isikamatwe Wakati Wakitengeneza Pombe

by I am Krantz
Feb 26, 2021
0

Nilizaliwa katika familia masikini sana na wakati...

Read more
Dkt. Ndungulile afurahishwa na huduma ya kufungua akaunti kidijitali kupitia SimBanking

Dkt. Ndungulile afurahishwa na huduma ya kufungua akaunti kidijitali kupitia SimBanking

Feb 26, 2021
Auto Draft

FAINALI NMB MASTABATA WIKI IJAYO, 424 WAZOA ZAWADI

Feb 24, 2021
Mamia wajitokeza kujisajili na Mbio za Kili Marathon Jijini Dar Es Salaam

Mamia wajitokeza kujisajili na Mbio za Kili Marathon Jijini Dar Es Salaam

Feb 23, 2021
BODI YA USAJILI WA WABUNIFU MAJENGO YAHAMASISHA WANAFUNZI KUPENDA FANI HIYO

BODI YA USAJILI WA WABUNIFU MAJENGO YAHAMASISHA WANAFUNZI KUPENDA FANI HIYO

Feb 23, 2021
Wateja wa Vodacom kuvuna Shilingi 4.1 bilioni za faida ya kutumia M-Pesa.

Wateja wa Vodacom kuvuna Shilingi 4.1 bilioni za faida ya kutumia M-Pesa.

Feb 23, 2021
Next Post
Serikali yapiga marufuku kanda ya ziwa kula nyama ya Nguruwe

Serikali yapiga marufuku kanda ya ziwa kula nyama ya Nguruwe

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

I agree to the Terms & Conditions and Privacy Policy.

Currently Playing

KRANTZ MWANTEPELE (FOUNDER & CEO)

ADVERTISEMENT

KONCEPT TV

https://www.youtube.com/watch?v=0HP0mB_rtIU&t=7s
Mwanaharakati Mzalendo

Mwanaharakati Mzalendo ni mtandao namba moja kwa habari makini kutoka pande zote za dunia kuhusiana na Michezo, Siasa, Afya, Elimu, Mahusiano, Vituko, n.k

Wasiliana nasi kwa Email;krantzcharles@gmail.com
SIMU; 0658123310

Follow Us

January 2021
M T W T F S S
« Dec   Feb »
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031
Currently Playing
  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

All rights reserved © 2020 Mwanaharakati Mzalendo - Powered by Koncept.

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv

All rights reserved © 2020 Mwanaharakati Mzalendo - Powered by Koncept.

Login to your account below

Forgotten Password?

Fill the forms bellow to register

*By registering into our website, you agree to the Terms & Conditions and Privacy Policy.
All fields are required. Log In

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In