Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene, amesema askari watakaoshindwa kuwabaini Wahamiaji haramu hususani maeneo ya mipakani wanapoingilia watawajibishwa.
Waziri Simbachawene amesema kitendo cha wahamiaji haramu kukamatwa maeneo mbalimbali ndani ya nchi, ambayo siyo mipakani ni kutokana na kuwepo na mawakala wanaofanikisha wahamiaji hao kuingia nchini.
Pia Simbachawene aliwataka wanafunzi wa Kambi hiyo kuzingatia masomo ya Kiuhamiaji wanayopewa yakiwemo ya uongozi na utawala, masuala ya kikonsula, mawasiliano, ulinzi wa kujihami na gwaride.
Akizungumza wakati akifungua mafunzo ya uongozi kwa maafisa na askari wa uhamiaji katika kambi mpya ya mafunzo ya Boma Kichaka Miba, iliyopo Wilayani Mkinga, Mkoa wa Tanga, Simbachawene amesema watawashughulikia askari wote wanaoingia katika mkoa ya mipakani ambapo wanaingia kwa mara ya kwanza wahamiaji hao.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa huo, Martine Shigela aliwataka waishio jirani na kambi hiyo kutoa ushirikiano na kambi hiyo, na pia wasivamie maeneo ya kambi hiyo ya Uhamiaji wakaona vichaka wakafikiri ni eneo ambalo halina mwenyewe na wakavamia.