Mfanyabiashara Elon Musk ambaye ni mmiliki wa kampuni ya kuten geneza magari ya umeme ya Tesla, amempiku mpinzani wake Jeff Bezos kwenye nafasi ya kwanza na kuongoza orodha ya matajiri duniani.
Musk alishilia nafasi pili kwa utajiri duniani, ameshika nafasi ya kwanza na kufikisha utajiri wa dollar za marekani Bilioni 191, akimzidi mpinzani wake Jeff Bezos ambaye ana utajiri wa dollar bilioni 184 kwa tofauti ya dollar bilioni 7.
Utajiri wa Musk umekua kwa kasi ya ajabu baada ya mauzo ya hisa za kampuni yake ya Tesla kukua kwa kasi katika soko la hisa duniani