Hospitali yatangaza kutoa matibabu bure siku ya Mapinduzi ya Zanzibar – Mwanaharakati Mzalendo
ADVERTISEMENT
  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact
Mwanaharakati Mzalendo
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv
No Result
View All Result
Mwanaharakati Mzalendo
No Result
View All Result
Home HABARI

Hospitali yatangaza kutoa matibabu bure siku ya Mapinduzi ya Zanzibar

Mhariri by Mhariri
Jan 9, 2021
in HABARI
0 0
0
Hospitali yatangaza kutoa matibabu bure siku ya Mapinduzi ya Zanzibar
0
SHARES
26
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Hospitali ya Elidad ya Boko Basihaya jijini Dar es salaam itaadhimisha sikukuu ya Mapinduzi ya Zanzibar (Januari 12) kwa kufanya vipimo vya afya bure kupitia kampeni ya Afya Bure.

Mkurugenzi Mtendaji wa hospiatli hiyo Dk Harry Matoyo alisema kuwa zoezi hili litafanyika Jumanne ijayo hospitalini hapo na siku hiyo watafanya uchunguzi wa magonjwa tofauti na kuwapa matibabu ya awali.

DK Matoyo alisema kuwa zoezi hilo litafanyika kuanzia asubuhi na watafanya uchuguzi wa magonjwa ya mifupa na viungo, uchunguzi wa magonjwa ya moyo na uchunguzi wa magonjwa wa kisukari.

Alisema kuwa wameamua kuadhimisha sikukuu hiyo kwa kutoa huduma bure ili kuunga mkono jitihada za Rais Dk John Magufuli za kuondoa adui maradhi ambayo serikali haitaweza kufanya peke yake.

ADVERTISEMENT

“Kuona kuwa serikali inapambana na adau maradhi, hospitali ya Elidad iliamua kuunga mkono serikali kwa kuanzisha Afya Bure Kampeni kwa lengo la kupambana na adui maradhi na kulijenga taifa lenye raia wenye afya njema,” alisema Dk Matoyo.

Alisema kuwa huduma ya vipimo na matibabu ya awali yataolewa kwa watu wenye rika zote na kuwataka wananchi kujitokeza siku hiyo kwani watakuwa na timu ya madakari wa kutosha.

Alisema kuwa hospitali ya Elidad ilianza mwezi Juni mwaka jana na kutoa matibabu ya magonjwa ya ujumla lakini ikijikita zaidi kwenye magonjwa ya mifupa yatokanayo na ajali na yasiyo ya ajali.“Pia tunatoa huduma za dharura (emergency), maabara, huduma za duka la dawa, huduma za physiotherapy, huduma za wagonjwa wa nje (opd), huduma za wagonjwa wa kulazwa (ipd), x ray, ultrasound, upasuaji wa aina mbalimbali na huduma za kutoa ushauri nasaa (counselling,” alisema dk Matoyo.

Kwa upande wake, Mkuu wa Utabibu wa hospitali hiyo Dk Cynthia Bashaija alisema kuwa kwa muda mfupi tangu waanze kutoa huduma wameweza kutambua kuwa siyo kila mtanzania ana uwezo wa kujifanyia uchunguzi na kuweza kutambua au kugundua magonjwa mbalimbali yakiwa katika hatua ya awali.

Dk Bashaija alisema kuwa wagonjwa wengi wamekuwa wakienda katika hospitali yao wakiwa katika hatua mbaya za mwisho na hivyo kufanya huduma za uponyaji kuwa ngumu na gharama zaidi.

“Aidha wapo wana nchi ambao hawaji hospitali kwa kuwa hawana uwezo na wengine ni kwasababu ya kupuuzia au uelewa mdogo. Kwa kuzingatia hilo, hospitali ya elidad imeona ina wajibu wa kuona taifa la Tanzania linakuwa na afya bora na kuanzisha kampeni hiyo,” alisema Dk Bashaija.

Alisema kuwa upimaji huo pia utahusisha kupima sukari, uzito, urefu, BMI, shinikizo la damu na magonjwa ya mifupa na hasa mgongo na magoti. Aliongeza kuwa zoezi hili lina lenga kugundua magonjwa hatua za awali na namna ya kuzuia hivyo haitahusisha gharama za matibabu hayo.

ADVERTISEMENT
Mhariri

Mhariri

Related Posts

Dkt.JPM ampongeza Mseveni kushinda Urais
HABARI

Dkt.JPM ampongeza Mseveni kushinda Urais

by Ombeni Osward
Jan 16, 2021
0

Rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania...

Read more
Raia wa Kenya ashikiliwa na TAKUKURU kwa kujaribu kumhonga apatiwe cheti cha COVID 19

Raia wa Kenya ashikiliwa na TAKUKURU kwa kujaribu kumhonga apatiwe cheti cha COVID 19

Jan 16, 2021
Nyumba 6 zaezuliwa na upepo mkali ulioambata na mvua mkoani Njombe

Nyumba 6 zaezuliwa na upepo mkali ulioambata na mvua mkoani Njombe

Jan 16, 2021
Mseveni ashinda Urais tena

Mseveni ashinda Urais tena

Jan 16, 2021
Bilioni 11 zaokolewa chakula cha Wafungwa

Bilioni 11 zaokolewa chakula cha Wafungwa

Jan 16, 2021
Waziri Ndugulile awataka wakuu wa Taasisi zilizochini yake kuwa wabunifu ili kuleta mafanikio

Waziri Ndugulile awataka wakuu wa Taasisi zilizochini yake kuwa wabunifu ili kuleta mafanikio

Jan 16, 2021
Next Post
Naibu Waziri Kipanga asimamisha kazi maafisa wanne VETA

Naibu Waziri Kipanga asimamisha kazi maafisa wanne VETA

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

I agree to the Terms & Conditions and Privacy Policy.

Currently Playing

KRANTZ MWANTEPELE (FOUNDER & CEO)

ADVERTISEMENT

KONCEPT TV

https://www.youtube.com/watch?v=0HP0mB_rtIU&t=7s
ADVERTISEMENT
Mwanaharakati Mzalendo

Mwanaharakati Mzalendo ni mtandao namba moja kwa habari makini kutoka pande zote za dunia kuhusiana na Michezo, Siasa, Afya, Elimu, Mahusiano, Vituko, n.k

Wasiliana nasi kwa Email;krantzcharles@gmail.com
SIMU; 0658123310

Follow Us

January 2021
M T W T F S S
« Dec    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031
Currently Playing
  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

All rights reserved © 2020 Mwanaharakati Mzalendo - Powered by Koncept.

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv

All rights reserved © 2020 Mwanaharakati Mzalendo - Powered by Koncept.

Login to your account below

Forgotten Password?

Fill the forms bellow to register

*By registering into our website, you agree to the Terms & Conditions and Privacy Policy.
All fields are required. Log In

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In